|
Wapiga picha wa kihistoria wa ZanzibarKaribu ya mwanzo wa karne iliyopita Mji Mkongwe wa Zanzibar ulikuwa ni bandari iliyojaa harakati, kitovu cha biashara, mtoaji wa kiungo cha mawasiliano na pia ulikuwa Mji wa Kimataifa. Wasafiri kutoka nchi mbali mbali walipita Zanzibar na kama walivyo watalii wa kileo walipenda kuweka kumbukumbu ya yale waliyoyaona . Kamera zilikuwa ni kubwa siku hizo, na ilikuwa vigumu kumiliki na kuzisafirisha. Lakini Zanzibar ilikuwa imebahatika kuwa na raia wenye maarifa, hamu ya biashara, mtazamo wa mbali na ujuzi wa kutosha wa kuweza kuingiza aina hizi za Kamera mpya katika visiwa hivi. Kamera hizi zilitumika kupiga picha matukio muhimu, majengo na mara nyengine 'rangi' za kienyeji ili kuziuza picha hizi kwa watu wenye shauku. Tumebahatika kwamba picha hizi nyingi tu zimeweza baadae kufanywa postikadi ambazo zipo hadi leo kutoa mwanga wa yaliyopita. Baadi ya machapisho ya sipia baadae yalipakwa rangi za mkono kama picha hizi za shirika kuu la kanisa la dayosisi ya Anglikana (UMCA Cathedral) iliyopigwa mwaka 1909.
Mitaa myembamba ya mji mkongwe wa waswahili imekuwa kila siku zikiwashangaza wageni na kwa hivyo, picha zake zimekuwa mauzo mazuri 1905. Wapiga picha wa Kizanzibari walijua umuhimu wa taswira na waliitumia ili kutengeneza picha za maajabu. 1905. Mji mkongwe ulikuwa na kiasi cha kampuni tatu za picha;
Hata leo katika maeneo ya maduka makongwe zipo picha zilizochanika za mviringo za mapaa ya mji mkongwe ambazo zinasemekana zimechukuliwa kutoka chumba cha kutimiza darubini "Camera Obscura" kilichojengwa na wapiga picha wa mwanzo kwenye mnara wa Beit el Ajaib.
Zipo mfano wa kazi nyengine nyingi za waasisi hawa bora wapiga picha wa kizanzibari katika Makumbusho ya Zanzibar. Makumbusho ya Zanzibar ipo kusini kidogo ya mji mkongwe, karibu na magereza. Nyaraka hizi nyingi ambazo zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza zipo wazi kwa uchunguzi wa kina kwa msaada wa wafanyakazi/waliosomea. Changia ukitembelea makumbusho.
Webmaster: Barghash@msn.com |