|
WAGOA NA ZANZIBARUwepo wa wagoa kisiwani Zanzibar ni wa mamia ya miaka hadi sasa. Ingawa mara nyingi ni katika idadi ndogo uwepo wa kudumu wa wafanyabiashara wa kigoa wenye vipaji, walimu, na mafundi stadi umewezesha kuacha kumbukumbu kubwa katika historia na jamii ya kizanzibar. Uwepo wa wagoa katika kipindi cha mwanzo upelelezi wa Afrika mashariki ni lazima ukumbukwe. Mnamo mwaka 1856 mpelelezi Richard Burton alisafiri hadi Bombay akiwa na Luteni Kamanda wake msaidizi Bwana John Hanning Speke ili kupata kibali cha Luteni Speke cha kuacha jeshi India. Huko Burton aliwachukua wagoa wawili kama wasaidizi katika safari nao walikuwa ni Valentine Rodrigues na Gaetano Andrade. Walisafiri pamoja na Burton hadi Zanzibar mnamo Desemba mwaka huo na mnamo Januari 1857 walimsindikiza katika safari fupi fupi za pwani wakienda Mombasa, Tanga na Pangani. Kisha mwezi Juni tarehe 16 walienda bara na baada ya kukodisha wapagazi zaidi Bagamoyo wao na takribani wengine 200 walitembea kuelekea katikati ya Afrika wakitafuta kuona chanzo cha mto Nile. Wagoa wote wawili waliweza kustahimili hii safari ya kuchosha ambayo ilidumu kwa taribani miaka miwili. Gaetano Andrade alikuwa ni mmoja wa watu 35 waliofanikisha ngwe ya mwisho wakiwa na Speke ambapo Burton aliugua. Hawa watu 35 walitembea maili za mwisho 226 kwa kipindi cha siku 25. Mwisho mnamo tarehe 3 1858 walisimama pamoja juu ya kilima wakaangalia bahari kubwa ndani ya bara ambayo Speke aliita Ziwa Victoria. Na huku Zanzibar katika mwaka 1859 pamoja na malalamiko ya Burton kuhusu utendaji wa baadhi ya wafanyakazi wake wakiwemo wagoa wawili, walilipwa mwishowe. Speke katika kujibu malalamiko haya alisema Ilikuwa ni rahisi kutenda haki ya kuwalipa kwa sababu walifuatana nasi hadi mwisho wa safari Pia alisema Valentine Rodrigues alijua kiswahili haraka na alikuwa msaada mkubwa katika kupika na kushona wakati Gaetano Andrade alikuwa muuguzi mpole na jasiri ingawaje alikuwa mdhaifu. Haijulikani kama Rodrigues na Andrade waliishi Zanzibar lakini ni wazi kwamba wagoa wengine waliwasili muda si mrefu baada yao kisiwani Zanzibar. Mwaka 1780 tabibu mwingereza aliandika kuwa kulikuwa na wagoa 31 waliokuwa wakiishi katika jiji la Zanzibar. Kabla ya sensa ya mwaka 1948 watu 598 wa asili kigoa walirekodiwa kuishi katika Kisiwa cha Unguja na wagoa 83 walirekodiwa kukaa Pemba. Hii inatupa jumla ya idadi ya wagoa Zanzibar katikati ya karne ya 20 kufikia 681. Wagoa waliiendelea kukimbilia Zanzibar kwa muda wa miaka mingine michache na kabla ya sensa iliyofuata mwaka 1958 ambapo makundi ya kikabila yalikatazwa na walipendelea zaidi kuandika mahali pa kuzaliwa na lugha ya kwanza mtu aliyoongea, familia asilia za kigoa hazikutambulika hivyo lakini bado kulikuwa na wakazi 313 wa kisiwa ambao walitambuliwa kama wazaliwa wa Kigoa na hata hao watu 85 walionesha Konkani ilikuwa ni lugha yao ya asili. Hawa walikuwa ni watu gani? Waliishije maisha yao? Zifuatazo ni picha na maelezo yakijaribu kutoa mwangaza kuhusu kundi hili dogo muhimu na labda kuchochea tafiti juu ya michango na harakati walizoendelea nazo wakati wa kuishi kwao kwa muda mrefu katika Afrika Mashariki. Katika mji wa zamani wa mawe palikuwa na kilabu cha jamaa wa kigoa na kilabu cha michezo cha kigoa lakini katikati ya jumuia kulikuwa Baada ya kujifunza dini, elimu ya mtoto ilipewa kipaumbele na jumuia ya kigoa hapo Zanzibar. Kwa hamasa kubwa walishiriki katika shughuli za ujenzi wa shule ya Mt. Joseph, walimu wengi walikuwa wagoa. Kulikuwa na na shule ndogo pia Pemba. Baada ya dini na elimu zilifuatia shughuli muhimu za maisha. Katika biashara hakuna aliyewashinda wafanyabiashara wa kigoa kwa utendaji, ubunifu na uchapakazi. Wagoa waliongoza katika nyanja zote za utawala serikalini na fani za kitaalam na hasa katika biashara. Usonara na Upigaji picha ni baadhi ya shughuli walizotawala humo visiwani. Mitaa ilijaa maduka ya wagoa ukiangalia katika picha zao za zamani. Mwisho katika utafiti wa makundi ya watu unazingatia zaidi kuangalia watu wenyewe hasa walio wawakilishi wa kundi hilo. Zifuatazo hapa chini ni historia za hao wawakilishi wachache.
Imeandikwa na kutayarishwa na Barghash@msn.com Haki zote zimehifadhiwa. Translated by Teacher George Mwidima, P.O. Box 60102 Dar es Salaam, Tanzania |