|
WANAWAKE WA ZANZIBARAkili na Nguvu Uzuri na Mitindohizi ni baadhi ya sifa walizopewa wanawake wa Zanzibar kihistoria. Sifa za nguvu, ujasiri na akili zao, ni vizuri zaidi ikiwa watazungumza wao wenyewe. Wanawake wa Zanzibar Zanzibar siku zote wametafuta njia wasikike kadiri wanavyokuwa wajuzi zaidi wa komputa/tarakilishi tutasikia mengi zaidi kutoka kwao kwenye mtandao pia. Kwa sauti zao wenyewe watazungumza wakiiambia dunia nzima. Watazungumzia urembo wao na ujuzi wa mitindo vilevile nahisi ninaweza nikatoa mifano michache na kuzungumza mimi mwenyewe. Mtu yeyote hawezi akaitembelea Zanzibar bila kuona wanawake wakupendeza wanaoishi katika visiwa hivi. Picha hapa chini zinaonesha wanawake wa kiZanzibari wa zamani. Kwa kupitia nyakati hizi tofauti, namna za uvaaji na kazi zao kubwa katika jamii, wote wanaonesha ile hamu ya kuishi, mtindo na msimamo wao kwangu unawaainisha wao ni wanawake wa Zanzibar asilia.
Siti Binti Saad Mama wa nyota wasanii maarufu. Wanamziki wote wa Taarab waliofuatia baada ya yeye kungara . Mwanamke wa mashuhuri, aliyejitahidi na kuweza kujiendeleza katika wakati huo kabla ya hata kuanza kuzungumzia masuala ya wanawake wa Afrika. Pia aliandika ushairi wa Busara na Hekima. Kwa maelezo zaidi kuhusu maisha yake, angalia http://groups.msn.com/SitiBintiSaad Zaidi ya miaka 90 ya muziki wa Zanzibar na historia imo kwa huyu Doyen wa Taarabu Bado anatumbuiza na hivi karibuni katika Tamasha la Filamu za Majahazi. Kwa maelezo zaidi angalia http://www.retroafric.com/html/sl_notes/012cd_3.html
Sayyida Salme, ni mmojawapo wa hao wanawake mashuhuri wa Zanzibar waliojitafutia mafanikio kwa mikono yao wenyewe. Kupitia vishawishi vingi katika maisha yaliyobadilikabadilika bado alisimama imara katika upendo wake kwa ajili ya Zanzibar. Kwa taarifa zaidi kuhusu huyu mtu muhimu kihistoria, angalia tovuti zifuatazo au andika kwa kwa taasisi ya Binti Salme London. http://www.proutworld.org/news/en/2001/jul/20010708vei.htm http://www.soas.ac.uk/gallery/Salme/home.html http://homes.hallertau.net/~alexbeck/bilder/sansibar/sansi.html http://www.zanzibar-web.com/salme.html https://www.nationalgeographic.de/php/magazin/topstories/2001/10/topstory1a.htm#head Bibi Henderson? Mke wa Bwan wa kiSkoti Sir John Henderson wa Fordel. Inasemekana kuwa amechukuliwa kutoka Zanzibar mnamo mwaka 1625, akifuatana na mjakazi wake. Kwa habari kamili bonyeza/bofya kiunganisho kifuatacho: http://www.travelintelligence.net/wsd/articles/art_52.html
Na Barghash 2002, imetolewa mahsusi kwa mke wangu. Translated by Teacher George Mwidima, P.O. Box 60102 Dar es Salaam, Tanzania |