|
MAPINDUZI YA SAA TISA
Zanzibar ni maarufu katika historia ya vita vifupi. Vita
vya karne ya 19 ambavyo vilimalizika kwa kiasi cha dakika 45 lakini vimetumika
kuonyesha mara zote ukatili kabla ya utawala wa ukoloni wa Ulaya Afrika
Mashariki. Kitu ambacho kinajulikana kwa uchache kabisa ni
kumbukumbu ya karne ya 20, ambapo Zanzibar ilishuhudia mfano wa vita
vifupi kabisa vya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika Mapinduzi haya, Serikali
ilidumu zaidi ya karne ilipinduliwa si chini ya siku moja. Taifa huru jipya la
Zanzibar la jamii ya kisultani inayojumuisha waarabu, wahindi, waswahili,
wangazija na wenyeji ikiongozwa na mrithi wa Sultani lilipotea kwa haraka ya
ajabu. Usiku huo ulitawaliwa na hali ya wasiwasi, kushangaza, ushupavu na kukata tamaa. Usiku huo ulianza saa tisa usiku. Kabla ya siku kuu kubwa ya kidini . Siku kuu hii iliwashajiisha makundi makubwa ya watu kukusanyika kuzunguka mji mkongwe. Watu walijenga mahema au kulala chini ya minazi huku wakisubiri ufunguaji wa sherehe wakati wa asubuhi. Baadhi ya makundi ya watu yalikuwa ni makundi ya vijana, baadhi ya vijana hawa walikuwa ni wafuasi wa mwanasiasa aliyejulikana kwa jina la John Okello. Suali la wafuasi wangapi walimfuata Okello katika mapinduzi hili ni suali la kutatanisha. Kwa hakika mwishoni mwa siku hiyo maelfu ya watu walijiunga na mapinduzi hayo baada ya kujulikana matokeo. Ni kweli kwamba, inasemekana kwamba Jemedari Mkuu Okello alikuwa na askari bataliani nne dhidi ya majeshi ya serikali usiku huo wa mapinduzi, lakini Jee, walikuwa watu wangapi wanapohisabiwa? Okello aliarifu kwamba mapinduzi yalianza usiku wa manane pale alipoachana na askari mia mbili na khamsini wa batalioni yake ya nne kwenye kambi ya Polisi ya Ziwani na ghala ya silaha. Saa tisa usiku alimrisha watu wake kukata waya wa ngome ya ziwani. Hilo lilikuwa tendo la mwanzo halisi la Kimapinduzi na lilisaidia kuwajua washiriki halisi wa Kimapinduzi. ("Separate the men from the boys"). Okello aliarifu juu ya watu wake wakati huo". Ukubwa wa kikwazo chetu ulikuwa wazi kwao. Tulikuwa tumejizatiti kwa mapanga, mikuki na vyuma vya magari na ulikuwa tunabahatisha kupambana uso kwa uso na askari waliosheheni bunduki za rashasha...." Wote waliondoka au kukataa kutambaa kupitia kwenye waya isipokuwa watu arubaini tu. Watu arubaini hawa ndio walioikamata Zanzibar na kuuangusha utawala wa Kisultani na zaidi ya miaka mia moja na thalathini na tatu kupitia masultani 12. Wanamapinduzi hawa walitambaa kiasi cha mita 25 ndani ya kambi ya Ziwani. Ndani walikuwepo maishirini ya maaskari. Askari hawa kama walivyo watu wengi wenye busara Zanzibar walikuwa wamelala ghorofa ya juu ambayo pepo baridi za bahari ziliweza kupoza/kuburudisha misitu ya joto. Askari wawili tu walikuwa macho na walikuwa wanashika zamu ya ulinzi chini. John Okello na askari wake waliwavamia walinzi hawa. Bunduki za rashasha zililia na watatu kati ya askari batalioni ya nne waliuliwa. Juu ya hivyo mmoja wa walinzi pia aliuawa, alimalizwa na mshale uliolengwa na Mwana Mapinduzi aliyeitwa Albert. Hapo tena Okello alikuwa uso kwa uso na mlinzi aliyebakia, ilikuwa hapa ndipo utabiri wa ushindi wa Mapinduzi ulipatikana. Watu hawa wawili walitwangana, Jemedari Mkuu anatwambia hivi" Nilimpokonya bunduki, tulipigana na kufanikiwa kumpiga tako la bunduki shavuni" Upigaji risasi ulisimama. Watu wa Jemedari Mkuu walikuwa tayari wamefika kwenye malango ya chumba cha silaha ambamo mamia ya Silaha za kisasa na maelfu ya risasi na baruti zilikuwa zimefungiwa. Askari wasiokuwa na silaha waliokuwa ghorofa ya juu, walijaribu kuteremka chini kwa fujo kwa kutumia ngazi moja tu ya nje huku wakiwa wamejaa wasiwasi. (kwa kudhibiti hali ya amani na utulivu ya kawaida, silaha zote hufungiwa kwa ajili ya kuzihifadhi wakati maofisa wa Polisi wanapokuwa hawapo kazini). Askari wa batalioni ya nne ya Okello walivurumisha mvua ya mikuki, mishale na mawe kwa askari walioduvaa na askari hawa wa Serikali walilundikana wenyewe katika ngazi nyembamba. Bunduki aliyoihodhi Okello ambayo ilikuwa na risasi tatu ilitumika kulengea risasi. Polisi hawa walirudi ghorofa ya juu kutafuta kamba ya kushukia kwa kupitia dirishani. Ilikuwa tayari wamechelewa, milango ya Chumba cha kuhifadhia silaha ilikuwa imevunjwa na Batalioni ya lnne walivamia ndani. Mara tu kila mmoja alikuwa yatari amesheheni bundundi ya rashasha. Wapiganiaji uhuru hawa ambao walianza usiku kwa silaha za vyuma vya magari zilizochongwa, sasa walikuwa ni jeshi lilsheheni silaha nzuri na bora. Askari hawa waliwasha moto wa ndege kwenye vyumba vya ghorofa ya juu na mara tu polisi waliobakia walisalimu amri. Askari wa Sultani walijaribu kujilinda vikali dhidi ya waasi hawa. Kikosi cha askari maalum chenye gari zenye kasi cha kukamata wahalifu kiliwasili kiasi cha saa baada ya ngome ya ziwani kukamatwa na wanamapinduzi. Askari hawa 75 walikuwa na bunduki nyepesi na walikuwa hawalingani na batalioni iliyosheheni silaha na iliyojidhatiti ndani ya ngome ya silaha. Waasisi waliachia askari wa Sultani kukaribia na baadae kuwa vurumishia mvua ya risasi. Mashambulizi yalikuwa makali sana hadi vichaka vya karibu vilishika moto, Polisi wa Sultani walirudi nyuma huku wakiwa wamekata tamaa.
Lakini juu ya hivyo hadi mchana Sultani alikuwa ameshakimbia nchi, iliyobakia ni historia tu. Na Barghash 2001 Barghash@msn.com |
|