Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

SKULI YA TUMEKUJA


HISTORIA FUPI YA SHULE YA SEKONDARI YA TUMEKUJA.

Ripoti hii ni kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa sasa wa Tumekuja:

Skuli inayo majengo makubwa matatu. Majengo mawili yenye Madarasa ya kusomea na Ukumbi wa Skuli. Kongwe kabisa ya majengo haya (lijulikanalo 19A) inaaminika kutumiwa na mmishionari wa Kifaransa AbbeFava. Jengo hili lilitumiwa kama ni kanisa dogo na makaazi ya watawala na "Sista wa Precious Blood" ("Sisters of the Precious Blood)" na lilitumika kama ni Skuli kwa Magoa, Maparisi, Wahindi na Watoto wanawake wa Kiafrika.

Na jengo lilikaribiana na hili lilijengwa kati ya mwaka 1890 - 1892 kama ni Hospital ya Kifaransa. Ilikuwa ndio Hospitali pekee ya kienyeji ya wazungu hadi 1911. Na baadae ikawa ni Ubalozi mdogo wa Uholanzi na makaazi ya wazungu kabla ya kuunganishwa na kufanywa Shule ya Kimisionari. (Jengo la Skuli ni hilo linaonekana kuliani kwenye picha ya 1905).

Ukumbi wa skuli ulijengwa mwaka 1956, na skuli hii iliendelea kutumika kama ni sehemu ya shule ya kimisionari ya Mtakatifu Joseph hadi kipindi cha Mapinduzi ya 1964. Wakati huu Skuli hii ilitaifishwa na Serikali na kuitwa jina la Skuli ya Tumekuja.

Mambo mengine muhimu yahusuyo Shule.

Skuli ipo katika eneo la mjini ikipakana na ofisi za Serikali. Skuli inazo sela ambazo inaaminika zilikuwa zikitumika kuwekea wafungwa wakati wa biashara ya Utumwa ya Afrika Mashariki. Jengo kuu la Skuli lina alama ya usanifu mzuri wa kuvutia wa kifaransa. Jengo hili lipo Kando ya Ukanda wa bahari na mara zote kunapatikana pepo baridi za baharini.

Hali ya Skuli ya Tumekuja sasa:

Skuli sasa inayo wanafunzi mia saba na arubaini. Lugha ya kufundishia katika shule hii ni kiingereza. Skuli hii ina vidato vinne kwa wanafunzi wa kawaida. Kila kidato kimoja kinachukua wanaufnzi 150. Skuli hii pia inayo aina nyengine ya wanafunzi ambao wanasoma mafunzo ya Biashara. Biashara na uwekaji hesabu, pamoja na masomo ya kawaida. Shule inayo kiasi cha wanafunzi 140 wa aina hii.

Idadi ya Waalimu: Idadi ya walimu ni 35. 23 ni wanaume na 12 ni wanawake.

Kadri ya umri wa wanafunzi: Umri wa wanafunzi ni kati ya miaka 14 - 19.

Idadi ya Madarasa:

Jengo kubwa lina madarasa 12. Yapo madarasa 17 yanayosomeshwa ambayo yanatumia madarasa haya kwa kubadilishana kipindi cha asubuhi na mchana. Skuli ilifungwa ili isitumike mwaka 1988 wakati mapaa yake yalipoangushwa na upepo mkali. Skuli ilifunguliwa tena mwaka 1992.

Matukio ya karibuni:

Mwaka huu tunatarajia kuwapata wahitimu wa kidato cha pili 154 na wahitimu 76 wa kidato cha nne. Wahitimu wa kidato cha nne wanaofanikiwa vizuri wanachaguliwa kuendelea na Sekondari za juu Zanzibar. Wahitimu wa kidato cha pili ambao wamepasi vizuri wanachaguliwa kujiunga na kidato cha tatu na wale ambao wamepasi vizuri zaidi wanachaguliwa kujiunga kidato cha tatu katika Sekondari za juu.


Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI

Na Barghash 2001 Barghash@msn.com