Zanzibar Yetu
Unguja na Pemba, Tumbatu na Mafia.
"Visiwa vilivyojitandaza kama kito katika upwa wa
Afrika"
Visiwa vikuu vya Zanzibar ni Unguja na Pemba, Tumbatu na Mafia. Mji
Mkongwe ulio katika ufukwe wa Magharibi ya kisiwa cha Unguja, ndio mji mkuu wa
eneo hili. Kwa hakika hasa, maeneo haya yamejengwa kwa miamba na chokaa, sio
mawe. Kwa sasa, kuna takriban majengo 1700 ya aina hii katika sehemu ya mji
mkongwe wa Zanzibar. Kati ya haya , 1100 yametambuliwa kama majengo yenye
thamani kubwa katika utaalamu wa ujenzi. Katika eneo
hili dogo, ambalo asili yake hasa kilikuwa kipande cha ardhi kilichozungukwa na
bahari mithali ya kisiwa kidogo, na ambalo ni kiasi cha eneo liingialo majengo
83 kwa vipimo vya mji, kuna chochoro 23, makanisa 2, zaidi ya misikiti 50,
Roshani 50, varandaa na baraza na
zaidi ya milango 200 iliyonakishiwa kistadi. Mji mkongwe wa Zanzibar
umechaguliwa kuwa "Eneo la urithi wa Kilimwengu" na Umoja wa Mataifa.
Umri hasa wa mji mkongwe haufahamiki. Je, uliibuka kutokana
na kijiji cha wavuvi kilichojulikana kuwepo katika kipande kihi cha ardhi tokea
karne ya 12, au mji huu ni mkongwe zaidi? Je, mji huu ni matokeo ya uhamiaji wa
karne ya 10 kutoka Uajeni" Au ni matokeo ya safari za karne ya 9 za
Maulamaa wa Kiislamu" Au makazi ya karne ya 1 ya Malkia Bilqis wa Shaba?
Mambo yote haya yanapendekezwa na wanahistoria kuwa yaweza kuwa tarehe ya kuanza
kwa mji huu. Ama twapaswa kuangalia nyuma zaidi, kiasi ya miaka 5000 hado 6000
iliyopita, pale wakaazi wa ndani ya
Bara la Afrika walipovuka bonde la ufa na kuanza kuvikalia visiwa vya Afrika Mashariki. Ni wao kweli
walioanzisha ustaarabu wa Madola ya mji ya visiwa kutoka lamu hadi Lindi? Je, ni
kweli kuwa visiwa hivi vya mji mkongwe vina mawanda ya takribani kilomita 1000?
Likiwa eneo kubwa kuliko yote la mji mkongwe ya waswahili,
Zanzibar ni sehemu bora kutembelea. Watalii sasa wanakaribishwa na huduma za
kitalii zimekuwa zikitanuliwa zaidi tokea miaka michache iliyopita. Hoteli na
nyumba za kulala wageni zinapatikana kwa bei unayoimudu. Kuna malazi kuanzia
ya gharama ndogo hadi yale ya kifahari. Uwanja wa ndege wa kimataifa upo
kilomita 5 tu kutoka mji mkongwe wenyewe na vyombo vingi vya kisasa, vya
baharini sasa hufanya safari kwa muda mchache tu baina ya visiwani na Bara. Kwa
wale wasiomudu kusafiri kwa sasa, basi nawafaidike kwa picha, vidokezo na habari
kuhusu Zanzibar, kihistoria na watu wake.
Webmaster: Barghash@msn.com