|
KITUO CHA ANGA ZANZIBAR
Kiasi cha kilomita 15 mashariki ya Mji Mkongwe, karibu ya kijiji cha Tunguu, yapo mabaki yaliyochakaa ya kituo cha Rada cha Kimarekani. Kituo hiki kilijengwa mwaka 1960 kwa ajili ya kunasia na kuwasiliana na misheni ya mwanzo ya kimarekani ya kwenda angani. Kituo hichi kilitumika kwa mara ya mwanzo wakati mradi wa mwanzo wa kwenda kwenye Sayari na "Mercury" ulipoanzishwa wakati wanaanga waliporuka katika Parabola yao kutoka Florida kwenda upande mwingine wa Afrika. Kituo hiki vile vile kipo mlalo wa njia ya dunia" Earth track" ya misheni za baadae za mzunguko kwenda kwenye Sayari na kwa hivyo kilikuwa kituo muhimu cha kunasia na pia cha upimaji na upitishaji wa data ambacho kilisaidia kuwasiliana na vyombo hivi vya Angani. Kituo hiki kilifungwa mara tu baada ya Mapinduzi ya 1964. Serikali mpya ya Mapinduzi ilidai kwamba Rada za kituo hich zingelitumika kuelekezea makombora Zanzibar. Wafanyakazi wa kituo hiki walihamishwa kwa haraka wakati huo chombo cha jeshi la wanamaji cha kimarekani (U.S Navy Destroyer) kilikuwa mbali kidogo na Mji Mkongwe kuhakikisha kwamba mafundi sanifu wa kimarekani na familia zao wanaondoka bila ya kusumbuliwa. Kwa leo ni tabu sana kugundua wapi kituo hiki kilikuwepo, lakini ikiwa utaelekea kusini kidogo ya njia kutoka Mji Mkongwe kuelekea mwambao wa Mashariki, kabla kidogo ya kufika Tunguu, mara tu utashtukia njia isiyoyakawaida iliyokaa sawa inayoongoza kuelekea kule ambako bado wenyeji za zamani wanaita majengo ya Wamarekani. "The Americani Buildings". Bora ya majengo haya yaliyohifadhiwa ni jengo la matengenezo la Mhudumu Mkuu (Butler - Aluminium Building) ambalo bado lina jenereta la dizeli ambalo lilikuwa linatumika kuendeshea kituo hiki cha Anga. Vile vile, karibu yake lipo Bweni (Dormitory building) ambalo lilikuwa linatumika na mafundi sanifu tu wakati misheni inatekelezwa. Wakati mwingine wamarekani hawa wote na familia zao waliishi karibu au ndani ya Mji Mkongwe ikiwa ni mchanganyiko wa jamii ndogo katika Zanzibar yenye mchanganyiko wa watu kutoka sehemu tofuati za dunia.
|