|
Ujasiri wa Zanzibar
Mshangao mkubwa katika Vita Fupi

Kasri la Zanzibar 1896, (Katikati) Jengo la Harem (kushoto) na Nyumba ya Maajabu
(kulia)
Muhtasari:
Vita katika mwaka 1896 kati ya Zanzibar na Uingereza imeandikwa kama tukio
fupi la kihistoria na mara nyingi limedharauliwa na kuchukuliwa kama mchezo wa
kuigiza ambao haustahili kufanyiwa utafiti wa kina. Historia ya vita hii hata
hivyo inaweza kuweka wazi mafunzo ya kudumu, na udogo wake kwa kweli unaweza
kuleta mtazamo kwa baadhi ya masuala makubwa yaliyopo wakati wowote vurugu za
kisiasa zikitokea.
Zanzibar
imeshindwa mara nyingi katika historia yake, lakini muda baada ya muda wenyeji
wenyewe wameweza kujiweka tena imara. Utulivu ungeweza kuwepo pale watu
wangejisikia wanaweza kuwahusisha katika mazungumzo ya maana kuhusu jinsi gani
wangetawaliwa na hata kuwa na sauti kuhusu nani awe miongoni mwa watu wanaongoza
Zanzibar. Maslahi haya muhimu yaligongana na maslahi yaliyokuwa wazi ya Ubeberu
wa Uingereza kwa wakati huo. Kwa namna fulani katika mgongano huo wa muda mfupi,
Zanzibar iliweza kutoa na kufikisha kilio chake cha kujiamini kinachosikika
katika historia nzima. Pamoja na ukubwa wa vurugu zilizonyamazisha sauti nyingi
za wa Zanzibari, ujumbe wake bado unaweza kusikika leo ukisikiliza kwa makini.
Jinsi ilivyokuwa:
Kabla ya adhuhuri tarehe
25, Agosti, 1896 Sayyid Hamid Thuwain bin Said, Sultan wa Zanzibar, Pemba,
Mafia, Lamu na sehemu zote za Syidi (Ukanda wa pwani ya Bara), alikufa. Kifo
chake kilianzisha mapambano mara moja kuwania kiti cha utawala miongoni mwa
familia za kiZanzibari.
Wakazi wa Omani, ikiwemo familia ya mtawala na
familia/koo nyingine maarufu zilikuwa na historia ndefu ya kujiamulia unapofika
wakati wa kuchagua mtawala mpya.
Desturi
hii iliimarishwa katika utaratibu wa kujenga maelewano baina ya koo
yaliyoendelezwa wakati wa kuchagua Imam katika nchi ya zamani (Oman) Huko nyuma
kabisa mwaka 751 Imam aliteuliwa na wakuu wa koo. Utaratibu huu wa kuchagua/maelewano
ulikuwa ni mojawapo ya mfano wa mwanzo wa aina fulani ya mfumo wa kidemokrasia
katika kipindi cha wanyanyasaji/madikteta.
Utaratibu wa kuachiana madaraka ya kisiasa Zanzibar ambao uliigwa kutoka
katika taratibu za uchaguzi za kidini uliweza kuharibiwa shughuli kubwa za
umwagaji damu. Ushindani miongoni jamii zinazotawala za vyama vyenye nguvu
uliweza kuwa mkali. Mwaka 1859 mfumo ulielezewa kama Warithi wote wa kiume
walikuwa na haki ya kuchaguliwa kuwa watawala...ikiwezekana, na kuchaguliwa na
kabila, ndio haki pekee. Sultan Barghash, alipoulizwa kuhusu taratibu za
kuachiana madaraka za Zanzibar aliweka wazi kwa ufupi kwa kusema haki ya kurithi
Taji la Uongozi litamwangukia mshindani yule tu mwenye Upanga Mrefu.

Mshindani mwenye upanga mrefu wakati Saayid Hamid alipokufa alikuwa waziwazi
ni Khalid bin Barghash. Kijana wa miaka 29, aliungwa mkono na wengi wa viongozi
wa biashara wa palepale na wamiliki ardhi wakubwa. Alikubalika kwa waHamadi wa
asili na waTumbatu na alikuwa ni mtoto wa ukoo bora. Hata hivyo hakukubalika kwa
waingereza.
Mtu wao alikuwa Hamoud bin Mohamed, mpwa wa aliyekuwa Sultan wa Oman na mtu
aliyependelea zaidi maisha ya kisasa. Waingereza walimuamini angeweza kuwa
rahisi zaidi kufanya naye kazi kuliko Khalid mwenye akili ya pekee ya
kujitegemea.
Familia za Kizanzibari hata hivyo ziliuona mwingilio huu wa waziwazi
katika taratibu zao uongozi kama fujo kwa utu wao na haki zao za kimila. Khalid
pia alikuwa mjukuu wa baba muasisi ya nchi, Sayyid Said. Alifaulu kuwa pamoja na
koo na watu wengi. Aliweza kuaminiwa na jeshi kubwa kisiwani na kabla ya saa
10:00 jioni siku hiyo ya Jumanne alitimiza majaribio ya mwisho ya kurithi
madaraka, alichukua Kasri/Ngome na kudhibiti bandari, Kikosi cha majahazi na
sehemu kubwa ya mji mkuu.
Waingereza
walikasirika. Walianza kujiandaa kwa ajili ya vita. Tayari kulikuwa na meli
mbili za kivita za Kifalme zimetia nanga katika bandari wakati Sultan
alipofariki. Serikali ya Uingereza ilimuagiza Mkuu wa Jeshi katika Bahari ya
Hindi kuharakishia Zanzibar na meli ya bendera na meli mbili za kivita zingine
za karibu zilielekezwa visiwani na amri ya kufika huko haraka iwezekanavyo.
Amri hiyo iliendelea hadi jioni ya Agosti tarehe 25, wanaume wa kiZanzibari
katika ua wa Kasri walikuwa na saa 40 kutafakari hatima yao. Ilikuwa kupigana au
kukimbia. Wangekaa? Wangeweza kweli kuendelea kusubiri tu na kukodoa macho kwa
Simba wa Ubereru ambaye alikuwa anakaribia kuachiliwa dhidi yao?
Majeshi:

Washikiliaji Mji/Wadhatiti
Katika
jiji majeshi wa Zanzibar yaligawanyika. Sultan wa zamani alikuwa na walinzi wa
kasri ambao walikuwa wamejiimarisha kwa kiasi kikubwa na kujirundikia silaha kwa
kipindi cha miaka michache ya utawala wake. Haya makundi yaliyogawanyika
yalisaidiwa na majeshi ya mizinga yaliyojaa waZanzibari, waarabu, wabaluchi na
wanamgambo wa Uajemi. (na inawezekana na baadhi ya wanamizinga wa Misri) Kwa
pamoja Jeshi la Ulinzi la Kifalme lilikuwa na jumla ya vikosi vipatavyo 1000.
Jeshi hili, kwa mtu mmoja, lilimwendea Khalid wakati mapambano kwa ajili ya
madaraka yalipoanza. Kwa ziada Khalid aliwaleta wasaidizi wapatao 300 pamoja
naye waliojipanga vizuri wakati alipoitwaa ngome. Mara aliposhikilia Ngome/Kasri
nayo madai ya waingereza yakajulikana, waZanzibari wengine 1,500 wakakimbilia
kwake. Hii ikafanya jumla ya vikosi 2,800. Wanaume wakajipanga kulinda Kasri,
Jengo la Harem lilikuwa karibu na uwanja uliokuwa mbele ya ua upande wa bahari.
Jeshi la majini la Zanzibar ambalo majahazi yake ya kivita kwa muda mrefu
yalikuwa yakidhibiti pwani ya Afrika Mashariki hadi muda huu yalikuwa yameuzwa
au kubadilishwa kwa matumizi ya kibiashara. Jeshi la waingereza la majini
lilikuwa limechukua jukumu la kutuliza ghasia katika Bahari ya Hindi.
Pia ufundi stadi wa Meli ya Mvuke ya Kivita iliyokuwa imenunuliwa kama Meli
ya Kibendera ya Sultan na chombo hiki H. H. S. Glasgow kilichopewa jina kufuatia
mahali kilipotengenezwa, kilisimama kimetia nanga bandarini. Wafanyakazi wa meli
Glasgow waliapa kiapo cha uaminifu kwa Sayyid Khalid akiwa kama Sultan wao mpya
na wakafyatua mizinga ya heshima kutoka katika mizinga ya zamani lakini ya
mizuri.
"Serikali"
Kwa
upande mwingine, vikosi vya Jeshi rasmi la Zanzibar (Serikali) vilikuwa na
idadi ya watu wapatao 900. Walikuwa wamejipanga katika vikosi viwili (pamoja
na bendi ) na viliongozwa na maafisa wa waingereza kama mkopo kwa Sultan wa
zamani. Kiongozi wa jeshi hili alikuwa ni mmojawapo wa aliyewahi kuwa afisa wa
jeshi la majini la uiengereza ambaye kwa miaka kadhaa sasa amekuwa msaidizi
katika serikali ya Zanzibar. Hadi kipindi hicho alikuwa amepandishwa cheo cha
Ujenerali wa Jeshi la Sultan. Jina lake lilikuwa Lloyd Mathews.
Mathews alivipa vikosi vyake mazoezi ya kutosha na vilionesha nidhamu na moyo
wa kupambana wakati wa safari za mara kwa mara pwani ambazo walizifanya kwa
maagizo ya serikali (na/au Mwingereza Mkazi). Pia mwanzoni walikuwa jeshi la
miguu bila silaha nzito.
Kulikuwa
na masuala mazito miongoni mwa wanadiplomasia waingereza kuhusu uaminifu kwa
vikundi hivi vya wafuasi na kwa kweli walionesha imani kidogo sana kwa
waingereza kuingilia kati. Vilevile walikuwa wataalam na Mathews kwa usahihi
alithibitisha kwamba watu wake wangefuata amri yoyote ambayo angewapa.
Wanadiplomasia hatimaye waliaamua wangejisikia salama zaidi na waliamini
wangeweza kuwa na uwezo zaidi kwa vikundi hivi , kwa kuviweka katika sehemu za
ulinzi, kusini ya Kasri/Ngome, kuzunguka sehemu ya diplomasia ya jiji.
Jeshi la Majini La Kifalme.
Zikiwa zimetia nanga bandarini wakati huo wa kifo za Sultan mwanzo zilikuwa
ni meli za waingereza H.M.S. Philomel na boti ndogo ya mizinga H.M.S. Thrush.
Ziliungana na meli nyenzake Thrush, H.M.S. Sparrow mnamo saa 11: 30 jioni.
Baadaye siku hiyo hiyo ya Jumanne jioni majeshi ya serikali mjini yaliongezewa
nguvu vikosi vya waingereza ambavyo havikutarajiwa vilivyoshuka kutoka katika
meli hizi. Vikosi vya majini vilikuja na mizinga fulani ya jeshi la majini, Kwa
kadirio la chini mzinga mmoja na machineguns (Maxim guns) mbili kubwa. Hizi mara
moja ziliwekwa kuzunguka Ubalozi wa Uiengereza.
Kisha vikosi vingine vya jeshi la majini vilianza kujikusanya. Nyingine
iliyofuatia kuonekana karibia saa 3:00 asubuhi siku ya Jumatano, ilikuwa meli
kubwa H.M.S. Raccoon na kisha adhuhuri mwezi Agosti tarehe 26, 1896 meli kubwa
sana Flagship H.M.S. Mt. George ilitia nanga katika bandari ya Zanzibar.
Kwa pamoja meli hizi tano zilibeba mizinga 78 mikubwa ya aina saba tofauti
tofauti, ikianzia mizinga ya mitutu 3 hadi ya inchi 9.2.
1. Mizinga 20 ya mitutu 3
2. Mizinga 12 ya mitutu 6
3. Mizinga 8 ya mitutu 9
4. Mizinga 12 ya inchi 4
5. Mizinga 8 ya inchi 4.7
6. Mizinga 16 ya inchi 6.0
7. Mizinga 2 ya inchi 9.2
Meli hizo zilikuwa ma bunduki mashine nzito na kila moja ilkuwa na milio
kadhaa na stendi ambazo rekodi za jeshi la majini zilizobebwa zingeweza kuwekwa.
Meli zilisogea pembezoni ufukoni , wakizunguka karibu sana na uzio ulioimarishwa.
Meli H.M.S. Sparrow ilimalizia siku ya pili ya mzozano ikatia nanga moja kwa
moja mbele ya kasri/Ngome, Meli H.M.S. Thrush ilikuwa mbali kidogo kaskazini
lakini karibu na ufukwe wa bahari, yadi 200 tu kutoka ukingo/ukuta wa bahari.
Kwa kweli hili lilikuwa jeshi kubwa sana la kutisha lililowahi kujikusanya
wakati huo katika Afrika Mashariki.
Nyakati zenyewe hasa:
Hatua ya Zanzibar kwa huu mkusanyiko wa majeshi ilikuwa kuendeleza mapambano
kwa upande mmoja na jitihada za kidiplomasia kwa upande mwingine. Uingereza
ilitoa waraka wa maandishi wa mwisho. Sultan Khalid aliambiwa kwamba lazima
aichie Ngome na atawanyike na majeshi yake au la sivyo uingereza imshambulie.
Alishauriwa zaidi na uingereza British kuwa "kuwa ameushikilia Usultani wa
Zanzibar bila ya kupata ushauri wao " alikuwa "ametenda kitendo cha uasi
dhidi ya serikali yake malkia tukufu ya Uingereza." Uingereza walikataa
kuzungumza na wasingewasiliana zaidi na majeshi ya waasi
Sayyid Khalid alijibu kuwa hatashambulia wazungu na alichotaka ni amani tu
kati yao. Pia alisema kuwa asingeweza kuicha ngome/kasri, " nyumba yake
na nyumba ya baba yake". Aliwasiliana na serikali za Ufaransa, Marekani
na Ujerumani kutafuta kupata kauli yao. Wote walikataa; Nchi hizi zote zilkuwa
na na makubaliano ya mkataba na Uingereza kwamba kwa njia moja au nyingine
kutojihusisha na lolote kwa Uingereza kuhusu masuala yote ndani ya makoloni yao.
Sultan alimuomba balozi wa Marekani kutoa taarifa kwa Malkia wa Uingereza.
Taarifa ilisomeka: " Malkia Victoria, London. Hamed bin Thweni amefariki.
Nimefanikiwa kuchukua kiti cha madaraka mababu zangu. Natumaini mahusiano ya
kirafiki yataendelea kama mwanzo. Khalid bin Barghash, Sultan." Taarifa
hii haikuwahi kufikishwa/kupelekwa.
Baadhi wametoa maoni kwamba jitihada zote hizi za kujiingiza katika biashara
ya umbali mrefu (bila shaka ndefu hasa) kampeni za kidiplomasia zinaonesha kuwa
waZanzibari hawakufahamu hatari ya mara moja na walikuwa wajinga kutotambua
jinsi gani silaha za Uingereza zilivyokuwa za hatari na jinsi gani jeshi la
majini lilivyokuwa tayari kuzitumia.
Dhana hii sio sahihi. Hakuna shaka kwamba uongozi wa Zanzibar ulijua kwa
undani jinsi gani majeshi ya waingereza yalivyoweza kuwa ya hatari kubwa. Tangu
zamani kabisa enzi za utawala wa mababu zake baadhi ya mawaziri wa Khalid's
walisafiri Ulaya na walitembelea viwanda vikubwa vya silaha vya mapinduzi
makubwa ya uundaji. Walikuwa miongoni mwao pia na miaka ya uzoefu wa
utengenezaji mizinga ya jeshi la majini na walikuwa wameona kwa macho yao
shughuli za jeshi la uingereza hivi karibuni katika bahari ya Hindi kwa makini
hasa.
Kwa
kuzingatia ukali wa vitisho vya waingereza, walipaswa kujua kuwa uingereza
haikuwa na mzaha/aibu kuhusu matumizi ya jeshi katika maeneo haya ya bahari
dhidi ya hao waliowapinga. Wote walijua mfano ulifanywa wa jiji la Alexandria
ambapo mwaka 1882, hili jiji lingine la mashariki lilishambuliwa kwa saa sita
mfululizo bila kupumzika na Jeshi la Maji la Uingereza. Huenda kulikuwa na
maveteran/wazoefu wachache wazee mingoni mwa wanamizinga wa kigeni wa Sultan
ambao walikuwa wameona hatua dhidi ya waingereza katika mapambano hayo miaka 14
hapo kabla.
Alexandria ulikuwa ni mji iliokuwa maarufu kwa harakati za utaifa za Misri
na kituo cha upinzani kwa serikali kibaraka iliyowekwa madarakani na Uingereza.
Wakati wanaharakati wa utaifa waliposhika udhibiti wa jiji meli kumi na tisa za
waingereza ziliwashambulia. Utayari/Nia ya meli za waingereza kushambulia katika
miji yenye wakazi wengi haikuwa tena mashakani katika sehemu hii ya dunia.
WaZanzibari walijua kikamilifu kitachogharimu msimamo wao kuendelea kupinga,
lakini bado walisubiri. Hakuna hata mtu mmoja aliyeondoka na kuiacha Ngome ile
iliyoimarishwa.
Usiku ulipoingia Khalid alitoka kwenda kwenye msikiti wa jamii kusali na
kuonesha alikuwa haogopi kutembelea mitaa. Na mara usiku ulipozidi kimya cha
kutisha kilitanda juu ya jiji. Baadhi ya mashahidi/waliokuwepo walisema kwamba
"hawajawahi kuona usiku mkimya wa namna hiyo". Mwingine aliandika kuwa "Ukimya
ulikuwa mkubwa na wa kutisha .....Kelele za hatua za miguu na sauti za
kutafunatafuna na kuongeaongea zilizofanywa na maelfu ya binadamu wakati wakila,
fanya kazi, cheza na kuzunguka zunguka: zote hizi zilitulia/nyamaza, na wakati
huo mji ulikuwa umejaa hofu na wasiwasi."
Mapigano:
Asubuhi
ya tarehe 27, ilikuwa nzuri na ilianza kuwa mbaya mapema wakati wananchi
walipojikusanya juu ya mapaa ya nyumba zao kutazama kitu gani kingetokea.
Viongozi wa Zanzibar tena walituma barua kwa wamarekani wakiomba wapeleke
telegraph London. Wawakilishi wa Marekani walikataa, wakisema kuwa "kama
Khalid hakutambuliwa kama Sultan na majeshi ya ulinzi ya Uingereza,
hata yeye hawezi kutambuliwa na mimi." Kwa lugha hiyo ya kidiplomasia
ilikuwa ndio nafasi ya mwisho iliyopotea ya kupatikana kwa amani iliyotolewa.
Maoni ya Marekani yalikwisha julikana kwa kazi hii ya suluhu iliyofanywa na
Zanzibar kwa sababu USA haikuwa mojawapo ya mataifa "yaliyopewa" sehemu ya
Afrika katika mkutano usio wa kinyama wa Berlin wa mwaka 1885. Vilevile wahusika
wakuu wa Marekani walikataa kupeleka taarifa au katika njia yoyote kuhoji haki
ya "Taifa lenye nguvu" kuwapeleka watu wa nchi hiyo katika kifo. Hii hasa
ilikuwa siku mbaya sana kwa harakati za kidiplomasia
Agizo/Tamko la mwisho la waingereza iliweka saa 3:00 asubuhi kama muda rasmi
kwa vita kuanza, Majeshi ya Majini yangeshambulia ikiwa majeshi katika Ngome/Kasri
yasingesalimu amri hadi wakati huo. Kabla ya saa yenyewe kuwadia tukio la
kijasiri lilitokea. Boti ndogo iliondoka katika uzio wa Zanzibar na kusogea
taratibu ikapita meli tatu za Uingereza. Mpango wake ulikuwa kumpeleka nahodha
wa Sultan katika meli yake pekee H.H.S. Glasgow. Meli hiyo ya kivita ya mbao
ilizungukwa na kubwa 5 zenye ngao lakini men watu waliokuwa ndani yake
hawakuhangaika kutia nanga wala kukimbia. Nahodha alipofika kwa nguvu walianza
matayarisho ya mwisho yaliyohitajika kufyatua mizinga yao ya zamani na
wakazilenga meli mbili za Uingereza zilizokuwa karibu. Waingereza waliona
kitendo hiki ni cha ukaidi na kwamba hakuna bendera iliyoshushwa na Zanzibari
asubuhi hiyo.

Kikosi cha meli cha Uingereza kilishambua kwanza, kwa usahihi kwa wakati huo
na moja kwa moja kwa wanaume wa kiZanzibari waliojikusanya ufukoni, Zanzibari
mara moja wakajibu mashambulizi. Mnamo saa 3:05, pamoja na sehemu yake ngumu,
meli H.H.S. Glasgow ilimfyatulia adui. Kisha waingereza wakaelekeza mashambulizi
mazito tokea pande zote mbili kwenye meli Glasgow. Ikiwa imetobolewatobolewa
karibu na mkondo wa maji mara moja ilianza kuzamishwa kwa kasi, huku ikifyatua
muda wote ilipokuwa ikienda chini ya maji.
Watazamaji walizikimbia paa wakati maganda yaliyorukaruka ovyo yalipopitiliza
na kutua juu ya uzio kabambe, yakiwasha moto sehemu kadhaa ndani ya jiji.
Watazamaji wale waliobaki juu waliweza, kwa muda mfupi, kuona moshi kutoka
tika mizinga katika pande zote mbili zikishambulia lakini muda si mrefu moshi
zaidi kutoka katika moto wa milipuko, ulifunika uzio wa Ngome/Kasri usiweze
kuonekana. Bado meli za waingereza ziliendelea kushambulia. Imekadiriwa kuwa
karibu ya maganda/mizinga elfu moja ilifyatuliwa Zanzibar siku hiyo. Ikiwa ni
kweli basi hiyo ina maana ganda lilianguka kwa kila baada ya sekunde tatu kwa
saa hiyo ya mashambulizi.
Kwa sababu ya maoni potofu maelezo mengi yanaangalia zaidi uzito wa
mapigano badala ya mafunzo yake. Shahidi mmoja atuambia kuwa "Kwa dakika
arobaini na tano kelele za kuogofya/ogopesha ziliendelea: miungurumo ya kuudhi,
iliyofutiwa na michakacho ya maxims (bunduki mashine) na mlio wa mtutu mmoja,
maganda yakilia hewani na vipandevipande vyake vikidondoka hapa na pale ovyoovyo."

Kabla ya saa 3:30 asubuhi Meli Glasgow jasiri ilikuwa kimya, mizinga yote
iliharibiwa na idadi kubwa ya waliokuwemo walikufa ama kujeruhiwa. Meli taratibu
ilizama kwenye kina kifupi cha kichanga cha bahari, milingoti yake bado
inaonekana juu ya maji. Mashambulizi kutoka kwa wazanzibari ufukweni yalipungua,
na bunduki zao za zamani moja baada ya nyingine zilichukuliwa. Mashambulizi ya
waingereza pia yalionekana kupungua wakati wafyatuaji waliposhindwa kuona
shabaha katika moshi na maafisa walianza kuangalia kama kuna dalili/ishara za
kusalimu amri. Ndani ya uzio liliweza kuonekana jengo la Harem lililokuwa
likiungua kwa moto mkali kwa kuwa kulikuwa na mabohari karibu na maji. Kisha
upepo uliupuliza moshi upande na hivyo kuruhusu muonekano mkubwa wa wahusika
wakuu wenye bendera wa Ngome/Kasri; wakiwa na bendera ya rangi nyekundu ya
Zanzibar bado ikipepea. Waingereza walirudia tena mashambulizi yao kwa nguvu
zaidi na tena mandhari punde tu ilifunikwa na moshi.
Baada
ya dakika nyingine 15 za mashambulizi, mashambulizi ya ulinzi upande wa
ufukweni yalikoma kabisa. Mizinga yote ya waZanzibari ilikuwa imeshatolewa nje
ya mapambano. Mashambulizi ya waingereza yalipungua na tena wahusika wakuu wa
bendera walionekana. Sehemu ya juu ilikuwa haionekani, Bendera ilikwanyuliwa
mbali. Mkuu wa Majeshi Rawlins, akiwa na majukumu katika kikosi cha jeshi la
majini, alichukulia hili kumaanisha kusalimu amri na aliamuru meli zake
kusitisha mapigano. Askari wa vikosi vya majini waliamriwa kuingia ndani,
kukamata sehemu zilizobakia za Kasri/Ngome kwa singe.
Aina fulani ya maelezo ya kutunga ya ya tukio hili la mwisho yalitolewa na
mwingereza akiandika mwaka mmoja tu baada ya vita hiyo.
"Kwa
makini Askari na waZanzibari ambao waliendesha mizinga ya mshikiliaji/mdhatiti
wa mji waendelea na kazi yao, na washambulia katika pande za boti za mizinga
bila kuonesha dhana yoyote ya udhaifu, mpaka vipandevipande kimoja baada ya
kingine vinatawanywa au kusambaa.
"Kwa kutokea nyuma kila moja ikilinda boti jasiri/bishi zilizojaa
zikilenga ...lakini kuingia kwa vikosi vyenye majaketi ya bluu hakuwi hivihivi
tu bila mapambano na upande mwingine wa pili. Hapa na pale milio ya mizinga na
bunduki, na kwa wakti huohuo idadi kubwa ya risasi zikidumbukia bila madhara
katika maji ya bluu ya bahari ya bandari, na chache zikipata nafasi miongoni mwa
waliokuwepo katika boti."
Matokeo:

Wakiwa bunduki zao zote lakini zilizoharibiwa na vikosi vya majeshi ya
maajini vya Uingereza wakija ufukweni kwa mamia, Khalid mara ya mwisho aliwapa
amri ya kuondoka katika uwanja wa mapambano. Wakiacha watu 500 wamekufa ndani na kribu ya ya Ngome, Sultan huyo
aliwahimiza wanamgambo wa wakiZanzibari kuwachukua waliojeruhiwa na kurudi nao
nyuma ya jiji walipotokea. Kisha akawaongoza watu wake waliobaki wakiwemo
walinzi wa ngome, katika matembezi ya hatari kupita jiji kulekea katika
Ubalozi Ujerumani. (na kuelekea katika majeshi ya kujitolea ambayo yalikuwa bado
hayajaruhusiwa kuondoka katika maeneo yao ya ulinzi.)
Shahidi mmoja ambaye alikuwa karibu na uwanja wa diplomasia aelezea tukio
hili: "Kilichokuwa cha kushangaza kwangu niliwapofikia wawakilishi kuona
idadi kubwa ya waarabu na wafuasi wao, wakiongozwa na Khalid, wote walijaa vumbi
na damu, wakija upande wangu na kuelekea katika Ubalozi wa Ujerumani."
Khalid alielekea njia yake akipita kundi moja la majeshi ya waingereza, ambayo
hayakumtambua, na alifikia sehemu maalum ya kufanyia mazungumzo. Wajerumani pale
walikuwa na sababu zao za kusaidia mpinzani wa waingereza na walimkaribisha na
idadi ndogo ya wasindikizaji wakuu. Wanajeshi wake mara walichukuliwa silaha zao
(na silaha zao ziliharibiwa) lakini baada ya hapo waliweza kuelekea na kupotelea
ndani ya kisiwa wakati majeshi ya serikali na vikosi vya uingereza vilitakiwa
kudhibiti mapigano ambayo yalitishia kuugubika mji na pia kushughulika na ghasia
zilizotokea mara matokeo ya vita yalipojulikana.
Sayyid
Khalid alibaki kwa siku 36 kama mgeni wa Baraza la Mazungumzo la Ujerumani.
Waingereza waliomba aletwe kwao na walilizunguka Baraza la Usuluhishi/Mazungumzo
wakiwa na wawakilishi na wanajeshi ili asiweze kukimbia. Baada ya majuma ya
mazungumzo ya Usuluhishi/Diplomasia kati ya nchi mbili za ulaya mwezi Oktoba
tarehe 2, asubuhi ya hasa kujaa kwa maji wakati bahari iliporusha maji kwenye
ukuta wa jengo la wajerumani, Khalid alitembea moja kwa moja kutoka katika
Baraza la Ujerumani kueleka katika boti ndogo, bila kugusa ardhi iliyokuwa sasa
inadhibitiwa na waingereza.
Kutokea
pale alipelekwa Dar es Salaam ambapo aliishi kama mwana wa Sultan mafichoni kwa
zaidi ya miaka 15 ambapo Vita ya kwanza ya dunia WW1 ilimleta tena kwenye
mzozo na Himaya ya waingereza. Habari hiyo itaendelea baadaye kama sehemu ya
pili ya hii Historia isiyo wazi ya majeshi ya Zanzibar.
Kwa
wakati huo kwa mji ulioharibiwa, Kasri/ngome iliharibiwa kabisa na haikujengwa
tena. Jengo la Harem pia liliharibiwa lakini jengo lingine la kurudishia mara
moja lilijengwa. Uharibifu katika Mnara wa kuongozea meli mbele ya Nyumba ya
Maajabu haukukarabatiwa lakini Beit el Ajaib (Nyumba ya Maajabu) yenyewe
haikuharibiwa sana hivyo mnara mwingine wa nyumba ya kuongozea meli uliongezewa
kwenye kasri/Ngone hiyo wakati lilipokarabatiwa mwaka 1899. Kabla ya mapema
miaka ya 1900 eneo lilikuwa tayari tena tayari kwa kuhudumia shughuli za umma/jamii
Vyombo
vya habari maarufu vya Uingereza viliiripoti vita kwa maelezo fulani ya kina kwa
wakati huo na hata nchini Marekani ilikuwa chini ya uchunguzi. Karibu na mwisho
wa mwaka 1896 jarida "Scientific American" lilichambua mbinu za mashambulizi.
Wakiwa na onyo la hatari za wazi zinazokuja, hatari ambazo Vita ya Kwanza ya
Dunia muda si mrefu vilidhihirisha , wamarekani walijaribu kutumia mafunzo
waliyojifunza Zanzibar katika mwambao wao wenyewe wa pwani.
"Mzinga wa inchi 6 wa kufyatua haraka kwenye meli ya Kifalme ya Arthur,
meli nyenzake St. George (Meli ya kubeba Bendera ya waingereza wakati wa vita ya
Zanzibar)... ina rekodi ya kumi na nane ya zilizolengwa katika muda wa dakika
tatu. Ikiwa kiwango hiki cha mashambulizi ya mapigo sita kwa dakika
ingeendelezwa kwa dakika thelathini na saba (muda uliofikiriwa wa vita )...
mzinga mmoja wa haraka ungerusha mizinga 222, ikiwa na uzito wa paundi 100 kwa
kila mzinga kulekea jijini. Meli ya St. George inabeba mizinga ya namna hiyo 5
kwenye sehemu yake pana...Pia iliweza kuleta (kwa wakati huo) mizinga fulani
mikubwa 120, ikiwa na uzito wa paundi 320 kwa kila moja, kutoka katika mizinga
yake ya inchi 9.2.
Ni
aina ya meli iliyotawanya majengo ya Zanzibar katika vipandevipande katika muda
usiozidi saa moja inamilikiwa na kila nchi inayomiliki jeshi la majini , kubwa
au dogo. Kwa hao watu ambao hawawezi kuona ulazima wa upinzani/ulinzi wa pwani
ya bahari unajirudiarudia kila sehemu, ukweli huu... utahakikisha mjadala huu wa
kusadikisha."
Alamo barani Afrika
Ujasiri
wa Zanzibar unaonekana ni aina fulani ya uhodari/ushujaa, uliojikita katika
imani kali ya usawa, na kanuni ya tabia fulani ujasiri. Tabia hizi , zikiwa
pamoja na ufahamu wa muda mrefu wa siasa wa watu wa Zanzibar, mara nyingi
umeyumbisha mipango ya wale ambao wangekuwa watawala waliojaribu kuvitawala
visiwa bila kujali maslahi ya wananchi.
Imesemekana vita hiyo fupi kabisa ilifanana na Mapinduzi ya Marekani ya mwaka
1776. Katika vita vyote wapiganaji walipinga haki ya Himaya ya waingereza
kutawala bila kuruhusu udhibiti mzuri wa kutosha wa mifumo ya jamii na uchumi wa
wazawa. Vilevile vita ya mwaka 1896 kati ya waingereza waZanzibari, ikiwa ya
pambano moja, labda ni vizuri zaidi kuifananisha na vita maarufu ya wamarekani
katika Alamo. Katika vita zote mbili, maelezo ya mapambano yamekuwa muhimu zaidi
kuliko matokeo ya mbinu zilizotumika.
Kwa hali hiyo kikundi kidogo cha wapiganaji wa Texas walichukua sehemu
muhimu zilizolindwa na walizitamisha chini rundo la bunduki za Jeshi lenye
nguvu la wamexico army bila kurudi nyuma. Kwa sababu ya kuzingatia kwao kanuni
za kujitegemea pamoja na kujiamini waliibuka washindi/mashujaa wa taifa.
Katika vita ya mwaka 1896 kikundi cha wapiganaji wa Zanzibari
walizitazamisha chini rundo la bunduki la majeshi ya waingereza na wengi wao
walikufa kuliko kukata tamaa katika nia yao. Hiyo ni simulizi ambayo haipaswi
kusahauliwa.
Mfano wao pia ni funzo wa kutafakari hata leo, wakati waZanzibari wapigana
na waZanzibari na majeshi yenye nguvu ya taifa na kimaitaifa yakishindana
kutawala eneo. Bila kufuatilia kwa makini/kwa karibu vilio hivi vya watu wa
visiwa hivi tutaona Alamo nyingine barani Africa?
Ifuatayo hivi karibuni:
Zanzibar na Vita Kuu: 1914-16
Bonyeza hapa upate Vyanzo na Maelekezo.
Sources and Bibliography

Webmaster:
Barghash@msn.com
![Hit Counter]()
Imetengenezwa mwaka 2002, kwa ajili ya Firdawsi na Mohammed.
Haki Zote Zimehifadhiwa.
Imetafsiriwa na Mwalimu George Mwidima
gmwidima@yahoo.com

|