Michoro ya Kale ya Zanzibar
Michoro ya W. A. Churchill.
William A. Churchill alikuwa jamaa mdogo wa Baraza la Ushauri la Waingereza
hapo Zanzibar mwishoni mwa miaka ya 1860's. Alikuja kwa ajili ya ziara visiwani
akileta kipaji chake tu na ubao wake wa kuchorea lakini hivi vilifanikisha
mwonekano fulani mzuri wa Zanzibar ya kale.
Reli ilioneshwa katika mchoro huu mzuri sio ile reli maarufu ya Bububu,
ambayo ilijengwa mwaka 1905 na ikaelekea kaskazini nje ya mji baada ya kupitia
karibu na N'Gambo. Kwa kiasi fulani ni reli ya zamani sana ambayo ilijengwa na Sultan Barghash.
Hii reli ya kipimo chembamba ilikuwa ni moja ya njia za mwanzo zilizotandazwa
katika Afrika ya kusini mwa Jangwa la Sahara. Ilielekea kusini ya mji kwenye
Ngome ya Sultan ya Chukwani. Mabehewa hapo mwanzoni yalivutwa na farasi wakati
reli ilipofunguliwa lakini mwaka 1881 injini ya kiberenge cha kwanza iliyowahi
kuingizwa Afrika Mashariki iliwasili kutokea Uingereza. Kiberenge hiki kiliitwa
"Sultanee" na kilivuta mabehewa katika reli hadi kilipofungwa/simamishwa mwaka
1892.
Katika mchoro huu Churchill aliweka picha ya mmoja wa wafanyabiashara wengi
kutoka dunia nzima ambaye alichukua makazi katika Zanzibar ya zamani.
Jeshi la Zanzibar halikuwa limewekwa vizuri nyakati zile, Jeshi la Majini
likiwa na kipau mbele zaidi kwenye vifaa bora na watu, lakini bado taratibu zake
za kuajiri za waziwazi zilisababisha jeshi kuwa angalau sehemu ya muda mfupi ya
wanajeshi wengi wataalamu wa umri huo.
Hata wanawake walifanya asilimia kubwa ya nguvukazi ambayo iliufanya Mji
Mkongwe
uendelee mbele kama jiji lifanyalo kazi lililotulia kwenye kingo za nyika kubwa
na kwa wakati huo sehemu kubwa ya nyika ya bara haikuwa imejulikana ambayo
ilikuwa Afrika ya zamani.
Baadhi ya wanawake wa Zanzibar wanaoneshwa kama ni watu wenye nguvu katika
jamii.
Miundo ya Serikali ilivutia Umakini wa Churchill.
Kama ambavyo alivyovutwa na matatizo ya watumwa na roho za majeshi ya Sultan.
Kabla ya mwishoni mwa miaka ya 1800's Livingston alionekana kama shujaa na
mjitoa mhanga nchini Uingereza.
Hili chapisho zuri lazima lingeuzwa sana.
Churchill alitumia ufundi fulani wa kisanii katika michoro yake (akionesha
labda bidii ya Mzoefu) lakini bado kazi zake nyingi zilikuwa za maisha ya kweli
hasa. Hapa chini ni baadhi ya picha za zamani za matukio kama hayo ambayo lazima
yatakuwa yamemwongoza katika michoro hii.
Ndugu wa W. A. Churchill alikuwa mwanadiplomasia bwana Henry Adrian Churchill
ambaye alikuwa mshauri wa Baraza la Zanzibar tokea mwaka 1867 hadi mwaka 1870.
H. A. Churchill alikuwa na kazi ya Udiplomasia kwa muda mrefu, alionekana
kuvutiwa katika kusaidia watu popote alipofanya kazi, aliandika makala kuhusu
kipindupindu hapo Zanzibar mnamo mwaka 1870, akiwasiliana na wanasayansi kuhusu
uwezekano wa matumizi ya ndege fulani wa kichina ili kupunguza makundi ya
mbung'o wa bara na alifanya kazi kama mkufunzi kwa ajili ya mtu maarufu zaidi wa
Baraza la Ushauri la Uingereza John Kirk, ambaye alimtumikia kama daktari wa
upasuaji na mshauri wake msaidizi miaka hiyo.
Kabla ya kuteuliwa kwake Zanzibar Churchill mkubwa alifanya kazi kama katibu na
mkalimani kwa wafanyakazi wa Kamishna/Mwakilishi wa Uingereza, akiwa na Jeshi la
Uturuki barani Asia, alishiriki katika ulinzi wa Kars, na alikuwa kwa muda
mfungwa wa Urusi. Nafasi yake ya mwisho alikuwa Mshauri wa Uingereza huko
Palermo mwaka 1879. Alifariki mwaka 1886.
Kidogo si dhahiri/wazi ni lini William alimtembelea kaka yake Zanzibar na
uchelewashaji mkubwa katika uchapishaji wa hii michoro ambayo haikuwekea sahihi
wala tarehe, (haikuchapishwa hadi mwishoni mwa miaka ya 1800's) yote haya
yanaifanya kazi ya kuiwekea tarehe michoro hii iwe ngumu. Mbali na hayo,
tukichukulia kuwa William hakukaa sana Zanzibar baada ya kuondoka kwa ndugu yake
kutokana na afya mbaya, basi naamini hizi ni mandhari za Zanzibar kuanzia
takribani mwaka 1870.
Imekusanywa na kuhaririwa na Barghash 2004.
Haki Zote Zimehifadhiwa.
Barghash@msn.com
Imetafsiriwa na George Mwidima
gmwidima@yahoo.com
|