Ghala ya Picha za A. C. Gomes
A. C. Gomes alianzisha studio ya picha Zanzibar labda
mapema sana mwaka 1868. Alikuwa na ushirikiano wa muda mfupi na J. B. Coutinho
katika miaka ya 1890. Mtoto wake wa kiume P. F. Gomes aliendeleza shughuli hiyo
ya kifamilia Zanzibar kwa miaka mingi, alifariki mwaka 1932. Kwa miaka yote hiyo
wote wawili wametuacha na baadhi ya picha za kuvutia.
Bonyeza kwenye mishale midogo pembeni ya safu ya juu ya
vipicha vidogo ili kuona mifano yote 9.
Kuendesha Chetezo kwa Upepo Zanzibar Jengo la Mawasiliano la Mashariki Garifahari la Farasi la Sultan
Wakati wa pepo za masika, kwenye mkondomaji wa Zanzibar, vifaa vyote vieleavyo vya kila aina viliweza kufikia/kwenda kasi kubwa. Picha hii baadaye ilitengenezwa stempu. Mtu ni lazima ashangae jinsi gani hasa picha hii ilivyochukuliwa/pigwa.
Kwa miaka mingi Mji Mkongwe karibu wote ulizungukwa na mikondo ya maji. Watu bado waligundua njia/namna za kutoka, kwenye hayo maji yaliyojaa au kupwa. Muziki na ngoma sikuzote zimekuwa sehemu ya utamaduni wa Zanzibar. Matanga ya majahazi ya zamani yaliungwaungwa pamoja na kukaa imara na yalikuwa katika hali ya kukarabatiwa karibu mara kwa mara. Mashua hii ya Taifa ilitumiwa mara kwa mara kumtoa Sultan nje ili kutembelea meli bandarini. Angeweza pia kuiagiza kwenda kivukoni kwa wageni muhimu watakao kumuona. Mizinga mbele ya Jela yaonesha kuwa picha hii ilichukuliwa punde tu baada ya Vita ya 1 ya Dunia. Kutoka katika sehemu hii ya kawaida waya nyingi za chini ya maji ziliunganishwa. Hii ilikuwa sehemu muhimu ya mtandao wa zamani wa mawasiliano duniani ambao uliruhusu mawasiliano ya haraka kati ya Ulaya na sehemu nyinginezo za dunia.
Asilimia kubwa ya watu wa visiwa walishiriki katika mavuno ya karafuu ya msimu. Kawaida ya muda maalum wa mavuno na idadi kubwa ya wavunaji iliyohitajika ilisababisha sehemu ya mavuno haya, kwa nyakati fulani, kuwa uwanja wa migogoro ya vibarua. Inasemekana kuwa garifahari hili la Farasi lilikuwa ni zawadi kutoka kwa Malkia Victoria.
Kuendesha Chetezo kwa Upepo Zanzibar
Wakati wa pepo za masika, kwenye mkondomaji wa Zanzibar, vifaa vyote vieleavyo vya kila aina viliweza kufikia/kwenda kasi kubwa. Picha hii baadaye ilitengenezwa stempu. Mtu ni lazima ashangae jinsi gani hasa picha hii ilivyochukuliwa/pigwa.
Kiasi kidogo cha historia ya familia kinaweza kuonekana
katika namna Gomes mkubwa alivyoziwekea lebo picha zake.
Kazi yake ya mwanzo kabisa ina alama ya Gomes and Company.
Kisha katika miaka michache twaona Gomes na Mtoto wa kiume.
Kisha mishowe twaona Gomes na Watoto wa kiume.
Kumbukumbu binafsi ya A. C. na P. F Gomes:
bonyeza kuikuza.
Imehaririwa mwaka 2004 na Barghash
Haki Zote Zimehifadhiwa:
Barghash@msn.com
Imetafsiriwa na George
Mwidima gmwidima@yahoo.com
|