| |
Ghala ya Picha za A. P. de Lord
Pereira de Lord na kaka yake walikuwa miongoni mwa
wapigapicha wabunifu zaidi katika historia ya Zanzibar. Hakuna mtu bado ana
kazi zaidi zilizohifadhiwa zinazopatikana leo kuliko wao, hii huenda ikawa ni
kwa sababu hakuna mtu mwingine alichukua/piga picha zaidi za Zanzibar ya zamani
kuliko wao.
Wanaonekana kuwa wamekuwepo kila mahali miaka ya mwanzoni,
katika mji mzima, nchini, baharini, katika majengo marefu na bila shaka
waliendeleza pia studio. Huko, mbali kidogo na mtaa mkuu katika Mji Mkongwe,
walitoa kumbukumbu nzuri kwa aina zote za wateja.
Jengo la Makazi na Zahanati ya Kifaransa
Bustani hizi zilibuniwa na kupandwa na wataalamu wa kiGoa na zilitolewa kwa jiji na Seyyid Hamoud mwaka 1899. Zilizopo karibu na njia kuu kuelekea jijini bustani hizo zilitumika kama sehemu ya kukutania na kupumzika ya watu wa daraja la juu. Barabara hii ya upande wa bandari imekuwa siku zote ni kiungo kikuu katika Mji Mkongwe. Garimoshi hili lilifanya kazi kwa chini ya miaka 20 lakini lilikuwa linapendwa sana na lilitumiwa sana na abiria. Hata hivyo upungufu wa misafara ya kutosha ya mizigo ulilifanya liwe ghali sana. Mipango ya kuliendeleza kuelekea upande wa kaskazini wa kisiwa haikufika mbali kulingana na Upimaji Ardhi na Ramani ya Njia. Mwonekano wa mchoro kwa nyakati fulani hukolezwa katika baadhi ya kazi za mwanzoni za deLords. Uendelezaji mdogo binafsi haukuathiri biashara ya picha, deLord alifungua duka katika sehemu iliyoonekana zaidi aliyoweza kuipata.
Ununuzi wa vitu maranyingi kwa pande zote mbili ni kazi na shughuli ya kijamii Zanzibar. DeLord alitumia rangi kupata mvuto wa kutosha wa mitindo ya mwaka 1910. Jengo kwa upande wa kushoto kabisa, hapa linatambuliwa kama Hospitali/Zahanati ya Kifaransa, baadaye likawa ni shule ya Mt. Joseph halafu likawa ni shule ya Tumekuja. Ukarabati wa meli ndogo na uungaji ulikuwa ni biashara yenye faida katika Zanzibar ya zamani.
Bustani hizi zilibuniwa na kupandwa na wataalamu wa kiGoa na zilitolewa kwa jiji na Seyyid Hamoud mwaka 1899. Zilizopo karibu na njia kuu kuelekea jijini bustani hizo zilitumika kama sehemu ya kukutania na kupumzika ya watu wa daraja la juu.
Imekusanywa na kuhaririwa na Barghash 2004
Haki Zote
Zimehifadhiwa. Barghash@msn.com
Imetafsiriwa na George Mwidima gmwidima@yahoo.com
|