Nyuma ya mapazia ya biashara kubwa zaidi ya kusafirisha nje viungo duniani kwa wakati huo kulikuwa na shughuli nyingi za kuchambua, kupanga, na kufungasha.
Mauzo ya karibia mazao yote yalifanywa kupitia mnada.
Pembe iliingizwa Zanzibar kisha ikatiwa dawa, na kutunzwa kwa usalama mpaka iliposafirishwa nje kuelekea mashariki (India na Uchina) na kuelekea magharibi (Uingereza na Marekani.)
Nchini Marekani mahitaji yalikuwa hasa makubwa, Massachusetts, viwanda vikubwa vilitengeneza marundo makubwa ya funguo za piano, vibanio vya nywele, mipini ya visu na mipira ya billiard.
Huduma hii ya kushangaza ya stoo ya muonekano wa kisasa inaonesha ni ya karibu na mwaka 1910. Zanzibar hadi wakati huo ilikuwa imetumika kwa muda mrefu kama kituo cha kuhidhia Mafuta na biashara Zanzibar ziliuza mafuta sehemu kubwa ya Afrika Mashariki.
Kabla ya paki za meli zilipojengwa kaskazini mwisho wa mji, mnamo mapema miaka ya 1920, sehemu kubwa ya mizigo kutoka katika meli zifikazo ilipakuliwa moja kwa moja kwenye ufukwe huu.
Hakuna hata mmoja anaweza jua tani ngapi zilihamishwa kwa mikono, kwanza kutoka katika meli kubwa kwenda kwenye boti ndogo na mitumbwi, kisha ufukweni, halafu juu mchangani kuelekea mjini, yote hayo kwa nguvu za wanaume na wanawake wa Zanzibar.
Visiwa vya Unguja na Pemba vilikuwa vimeshafunikwa na minazi milioni nne. Kulikuwa na mashamba ya miti mikubwa ambayo yalikuwa yakisaidiwa na soko linashamiri kwa ajili ya copra. Leo kuna miti michache na karibu hakuna soko la kupeleka nje kwa bidhaa za nazi.
Kulikuwa na mashirika kadhaa ya kisheria hapo Zanzibar ya zamani na mahakama katika Mji Mkongwe yaliyokuwa kazini sikuzote kusikiliza kesi zote muhimu, zote za madai na jinai. Kulikuwa na hata Mahakama Kuu Zanzibar ambayo ilikuwa maalum kwa sheria za usafirishaji melini.
Kwa hao wanaowasili kwa meli, wafanyabiashara wa kwanza wa Zanzibar waliokutana nao walikuwa maranyingi wavulana ndani ya boti ndogo. Wangeonesha uwezo wao wa kuchupa/kupiga mbizi kwenye vina vikubwa kufuatilia sarafu zilizotupwa na abiria.
Harji pia alipenda kupiga picha matukio ya umati. Maranyingi aliziwekea rangi hizi picha kupata kikolezo cha kufurahisha cha matukio.
Julai 27, 1902. Watu wanasubiri kuwasili kwa Sultan mpya. Huyo angeshakuwa Sayyid Ali Bin Hamoud ambaye alikuwa mbali wakati Sultan mzee alipokufa.
Inasemekana kuwa mtawala mpya mwenye mshawasha na umri mdogo, ambaye alikuwa akirejea Zanzibar baada ya miaka 3 nchi za nje katika shule ya bweni, alizidiwa sana na Kifo ambacho hakikutarajiwa cha baba yake na makundi ya watu makubwa wakati wa kuwasili kwake kiasi Sayyid Ali alikuwa hawezi kuzungumza kwa siku mbili.
Hakuweza kuhutubia kundi kubwa la watu walioneshwa katika hii picha iwekewayo rangi kwa nadra. Waliondoka wakiwa wamehuzunishwa, bahati mbaya labda kwa enzi mpya ya utawala. Sultan Ali baadaye akawa Sultan wa Zanzibar pekee aliyewahi kung'atuka.