Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

Wapiga picha wa kihistoria wa Zanzibar


Karibu ya mwanzo wa karne iliyopita Mji Mkongwe wa Zanzibar ulikuwa ni bandari iliyojaa harakati, kitovu cha biashara, mtoaji wa kiungo cha mawasiliano na pia ulikuwa Mji wa Kimataifa. Wasafiri kutoka nchi mbali mbali walipita Zanzibar na kama walivyo watalii wa kileo walipenda kuweka kumbukumbu ya yale waliyoyaona .

Kamera zilikuwa ni kubwa siku hizo, na ilikuwa vigumu kumiliki na kuzisafirisha. Lakini Zanzibar ilikuwa imebahatika kuwa na raia wenye maarifa, hamu ya biashara, mtazamo wa mbali na ujuzi wa kutosha wa kuweza kuingiza aina hizi za Kamera mpya katika visiwa hivi. Kamera hizi zilitumika kupiga picha matukio muhimu, majengo na mara nyengine 'rangi' za kienyeji ili kuziuza picha hizi kwa watu wenye shauku. Tumebahatika kwamba picha hizi nyingi tu zimeweza baadae kufanywa postikadi ambazo zipo hadi leo kutoa mwanga wa yaliyopita.


Baadi ya machapisho ya sipia baadae yalipakwa rangi za mkono kama picha hizi za shirika kuu la kanisa la dayosisi ya Anglikana (UMCA Cathedral) iliyopigwa mwaka 1909.

Mitaa myembamba ya mji mkongwe wa waswahili imekuwa kila siku zikiwashangaza wageni na kwa hivyo, picha zake zimekuwa mauzo mazuri 1905.

Wapiga picha wa Kizanzibari walijua umuhimu wa taswira na waliitumia ili kutengeneza picha za maajabu. 1905.

Mji mkongwe ulikuwa na kiasi cha kampuni tatu za picha;

  • Kampuni ya Continho Bras; (Ambayo baadae ilifanyakazi kwa jina la J.B Countiho, Wapiga picha, Zanzibar).

Ghala la Picha za Coutinho

  • Kampuni ya A.C Gomes and Sons.

Ghala za Gomes

  • Kampuni ya Pareira de Lord Brothers (Wapiga picha na wasanii, Zanzibar).

Ghala za deLord

  • Karim Essa Allibhai

  • Ali Pira Harji



Ghala la Picha za Harji


Hata leo katika maeneo ya maduka makongwe zipo picha zilizochanika za mviringo za mapaa ya mji mkongwe ambazo zinasemekana zimechukuliwa kutoka chumba cha kutimiza darubini "Camera Obscura" kilichojengwa na wapiga picha wa mwanzo kwenye mnara wa Beit el Ajaib.

Zipo mfano wa kazi nyengine nyingi za waasisi hawa bora wapiga picha wa kizanzibari katika Makumbusho ya Zanzibar. Makumbusho ya Zanzibar ipo kusini kidogo ya mji mkongwe, karibu na magereza. Nyaraka hizi nyingi ambazo zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza zipo wazi kwa uchunguzi wa kina kwa msaada wa wafanyakazi/waliosomea. Changia ukitembelea makumbusho.


Webmaster: Barghash@msn.com

Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI