Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
كشف النقاب عن زنجيبار
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

MAPINDUZI YA SAA TISA

 


    

 

Zanzibar ni maarufu katika historia ya vita vifupi. Vita vya karne ya 19 ambavyo vilimalizika kwa kiasi cha dakika 45 lakini vimetumika kuonyesha mara zote ukatili kabla ya utawala wa ukoloni wa Ulaya Afrika Mashariki.

Kitu ambacho kinajulikana kwa uchache kabisa ni  kumbukumbu ya karne ya 20, ambapo Zanzibar ilishuhudia mfano wa vita vifupi kabisa vya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika Mapinduzi haya, Serikali ilidumu zaidi ya karne ilipinduliwa si chini ya siku moja. Taifa huru jipya la Zanzibar la jamii ya kisultani inayojumuisha waarabu, wahindi, waswahili, wangazija na wenyeji ikiongozwa na mrithi wa Sultani lilipotea kwa haraka ya ajabu.

Usiku huo ulitawaliwa na hali ya wasiwasi, kushangaza, ushupavu na kukata tamaa. Usiku huo ulianza saa tisa usiku. Kabla ya siku kuu kubwa ya kidini . Siku kuu hii iliwashajiisha makundi makubwa ya watu kukusanyika kuzunguka mji mkongwe. Watu walijenga mahema au kulala chini ya minazi huku wakisubiri ufunguaji wa sherehe wakati wa asubuhi. Baadhi ya makundi ya watu yalikuwa ni makundi ya vijana, baadhi ya vijana hawa walikuwa ni wafuasi wa mwanasiasa aliyejulikana kwa jina la John Okello.  Suali la wafuasi wangapi walimfuata Okello katika mapinduzi hili ni suali la kutatanisha.

 

Kwa hakika mwishoni mwa siku hiyo maelfu ya watu walijiunga na mapinduzi hayo baada ya kujulikana matokeo. Ni kweli kwamba, inasemekana kwamba Jemedari Mkuu Okello alikuwa na askari bataliani nne dhidi ya majeshi ya serikali usiku huo wa mapinduzi, lakini Jee, walikuwa watu wangapi wanapohisabiwa?

 

Okello aliarifu kwamba mapinduzi yalianza usiku wa manane pale alipoachana na askari mia mbili na khamsini wa batalioni yake ya nne kwenye kambi ya Polisi ya Ziwani na ghala ya silaha.   Saa tisa usiku alimrisha watu wake kukata waya wa ngome ya ziwani.  Hilo lilikuwa tendo la mwanzo halisi la Kimapinduzi na lilisaidia kuwajua washiriki halisi wa Kimapinduzi. ("Separate the men from the boys").  Okello aliarifu juu ya watu wake wakati huo".  Ukubwa wa kikwazo chetu ulikuwa wazi kwao.  Tulikuwa tumejizatiti kwa mapanga, mikuki na vyuma vya magari na ulikuwa tunabahatisha kupambana uso kwa uso na askari waliosheheni bunduki za rashasha...." Wote waliondoka au kukataa kutambaa kupitia kwenye waya isipokuwa watu arubaini tu.  

Watu arubaini hawa ndio walioikamata Zanzibar na kuuangusha utawala wa Kisultani na zaidi ya miaka mia moja na thalathini na tatu kupitia  masultani 12.

 

Wanamapinduzi hawa walitambaa kiasi cha mita 25 ndani ya kambi ya Ziwani.  Ndani walikuwepo maishirini ya maaskari.  Askari hawa kama walivyo watu wengi wenye busara Zanzibar walikuwa wamelala ghorofa ya juu ambayo pepo baridi za bahari ziliweza kupoza/kuburudisha misitu ya joto.  Askari wawili tu walikuwa macho na walikuwa wanashika zamu ya ulinzi chini.

 

John Okello na askari wake waliwavamia walinzi hawa.  Bunduki za rashasha zililia na watatu kati ya askari batalioni ya nne waliuliwa.  Juu ya hivyo mmoja wa walinzi pia aliuawa, alimalizwa na mshale uliolengwa na Mwana Mapinduzi aliyeitwa Albert.  Hapo tena Okello alikuwa uso kwa uso na mlinzi aliyebakia, ilikuwa hapa ndipo utabiri wa ushindi wa Mapinduzi ulipatikana.  Watu hawa wawili walitwangana, Jemedari Mkuu anatwambia hivi"  Nilimpokonya  bunduki, tulipigana na kufanikiwa kumpiga tako la bunduki shavuni"  Upigaji risasi ulisimama.  Watu wa  Jemedari Mkuu walikuwa tayari wamefika kwenye malango ya chumba  cha silaha ambamo mamia ya Silaha za kisasa na maelfu ya risasi na baruti zilikuwa zimefungiwa.  Askari wasiokuwa na silaha waliokuwa ghorofa ya juu, walijaribu kuteremka chini kwa fujo kwa kutumia ngazi moja tu ya nje huku wakiwa wamejaa wasiwasi.  (kwa kudhibiti hali ya amani na utulivu ya kawaida, silaha zote hufungiwa kwa ajili ya kuzihifadhi wakati maofisa  wa Polisi wanapokuwa hawapo kazini).  Askari wa batalioni ya nne ya Okello walivurumisha mvua ya mikuki, mishale na mawe kwa askari walioduvaa na askari hawa wa  Serikali walilundikana wenyewe katika ngazi nyembamba.  Bunduki aliyoihodhi Okello ambayo ilikuwa na risasi tatu ilitumika kulengea risasi.  Polisi hawa walirudi ghorofa  ya juu kutafuta kamba ya kushukia kwa kupitia dirishani.

 

Ilikuwa tayari wamechelewa, milango ya Chumba cha kuhifadhia silaha ilikuwa imevunjwa na Batalioni ya lnne walivamia ndani.  Mara tu kila mmoja alikuwa yatari amesheheni bundundi ya rashasha.  Wapiganiaji uhuru  hawa ambao walianza usiku kwa silaha za vyuma vya magari zilizochongwa, sasa walikuwa ni jeshi lilsheheni silaha nzuri na bora.  Askari hawa waliwasha moto wa ndege kwenye vyumba vya ghorofa ya juu na mara tu polisi waliobakia walisalimu amri.

 

Askari wa Sultani walijaribu kujilinda vikali dhidi ya waasi hawa.  Kikosi cha askari maalum chenye gari zenye kasi cha kukamata wahalifu kiliwasili kiasi cha saa baada ya ngome ya ziwani kukamatwa na wanamapinduzi.  Askari hawa 75 walikuwa na bunduki nyepesi na walikuwa hawalingani na batalioni iliyosheheni silaha na iliyojidhatiti ndani ya ngome ya silaha.  Waasisi waliachia askari wa Sultani kukaribia na baadae kuwa vurumishia mvua ya risasi.  Mashambulizi yalikuwa makali sana hadi vichaka vya karibu vilishika  moto, Polisi wa Sultani walirudi nyuma huku wakiwa wamekata tamaa.

  Kwa kutumia  kituo chao hiki kipya, wanamapinduzi walitawanya bunduki  kwa batalioni nyengine tatu (ambazo tayari zilikuwa zimeshazizunguka sehemu muhimu lakini bado kuzishambulia.  Kwa amri ya mara moja vituo vyengine vya Polisi na mawasiliano vilishambuli na kukamatwa.  Upinzani mkubwa ulikuwa kituo cha Polisi cha Malindi, ambapo hadi asubuhi lmilio ya risasi ilisikika.

 

 

Lakini juu ya hivyo hadi mchana Sultani alikuwa ameshakimbia  nchi, iliyobakia ni historia tu.


                     Na Barghash 2001 Barghash@msn.com

Up Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO  CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI