KITUO CHA ANGA ZANZIBAR
Kiasi
cha kilomita 15 mashariki ya Mji Mkongwe, karibu
ya kijiji cha Tunguu, yapo mabaki yaliyochakaa ya kituo cha Rada cha
Kimarekani. Kituo hiki kilijengwa
mwaka 1960 kwa ajili ya kunasia na kuwasiliana na misheni ya mwanzo ya
kimarekani ya kwenda angani. Kituo hichi kilitumika kwa mara ya mwanzo wakati mradi wa
mwanzo wa kwenda kwenye Sayari na "Mercury" ulipoanzishwa wakati
wanaanga waliporuka katika Parabola yao kutoka Florida kwenda upande mwingine wa
Afrika. Kituo hiki vile vile kipo
mlalo wa njia ya dunia"
Earth track" ya misheni za baadae za mzunguko kwenda kwenye Sayari na kwa
hivyo kilikuwa kituo muhimu cha kunasia na pia cha upimaji na upitishaji wa data
ambacho kilisaidia kuwasiliana na vyombo hivi vya Angani.
Kituo hiki kilifungwa mara tu baada ya Mapinduzi ya 1964.
Serikali mpya ya Mapinduzi ilidai kwamba Rada za kituo hich zingelitumika
kuelekezea makombora Zanzibar. Wafanyakazi
wa kituo hiki walihamishwa kwa haraka wakati huo chombo cha jeshi la wanamaji
cha kimarekani (U.S Navy Destroyer) kilikuwa mbali kidogo na Mji Mkongwe
kuhakikisha kwamba mafundi sanifu wa kimarekani na familia zao wanaondoka bila
ya kusumbuliwa.
Kwa
leo ni tabu sana kugundua wapi kituo hiki kilikuwepo, lakini ikiwa utaelekea
kusini kidogo ya njia kutoka Mji Mkongwe kuelekea mwambao wa Mashariki, kabla
kidogo ya kufika
Tunguu, mara tu utashtukia njia isiyoyakawaida iliyokaa sawa
inayoongoza kuelekea kule ambako bado wenyeji za zamani wanaita majengo
ya Wamarekani. "The Americani
Buildings". Bora ya majengo haya yaliyohifadhiwa ni jengo la matengenezo la
Mhudumu Mkuu (Butler - Aluminium Building) ambalo bado lina jenereta la
dizeli ambalo lilikuwa linatumika kuendeshea kituo hiki cha Anga.
Vile vile, karibu yake lipo Bweni (Dormitory building) ambalo lilikuwa
linatumika na mafundi sanifu tu wakati misheni inatekelezwa.
Wakati mwingine wamarekani hawa wote na familia zao waliishi karibu au
ndani ya Mji Mkongwe ikiwa ni mchanganyiko wa jamii ndogo katika Zanzibar yenye
mchanganyiko wa watu kutoka sehemu tofuati za dunia.




|