WAZANZIBARI MAARUFU
TIPPU TIP
Akiwa
ametiwa ila sana na "magazeti ya wavumbuzi," shujaa huyu jasiri wa
kizanzibari ambaye jina lake hasa aliitwa Hamed bin Mohammed Marjebi alijulikana
zaidi kama Davy Corocket au Francis Drake wa Afrika ya Mashariki kuliko
mfano wa mwanafunzi mtundu ambaye tabia zake zilizompa umaarufu zaidi ni
vile kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na wavumbuzi wa kidini kutoka Ulaya wa
wakati ule. Aliwatumikia Sultani
wake kwa zaidi ya miaka 50, huku akibeba bendera na ustaarabu wao katika kila
pembe ya mipaka yao.
Katika nyakati tafauti, alifanya kazi kama mvumbuzi,
kiongozi, mfanyabiashara, askari mwanadiplomaisa, hakimu na gavana.
Aliwatumikia jumla ya Sultani 8 wakati wa maisha yake baadaye akastaafu
na kubakia nyumbani kwake katika Mji Mkongwe.
Alifariki mwaka 1905 akiwa hakuwahi kuhalifu kazi zote alizopewa na
watawala wake.
SITI BINTI SADI.
Akiwa
Nyota wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab tokea miaka ya mwanzo ya santuri, Siti
aliweza kuifanya Taarab kuwa maarufu kutokana na muziki wake mtamu na nyimbo za
mapenzi zilizobeba ujumbe wa nguvu za kijamii na uchambuzi wakisiasa.
Jambo moja lililoifanya kazi yake kuwa ya kiharakati ni vile kuimba kwake
kwa kutumia lugha ya watu wa kawaida. Baada
ya kuishi kwa muda mrefu katika mitaa ya Ng'ambo mjini Zanzibar, baadaye Siti
alitembelea nchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki akiimba na kuuza rekodi zake.
Lililompa umaarufu zaidi miongoni mwa watu ilikuwa ni muziki mpya
uliorekodiwa katika lugha yao wenyewe. Baada
ya wasomo wanadai kuwa rekodi hizi za zamani zilichangia sana
kuieneza lugha ya Kiswahili.
Akiwa mtoto wa watumwa, Siti alianza
maisha kwa akali ya kitu, lakini kwa juhudi yake mwenyewe na sauti
yake ya ajabu, aliweza kwanza kuimba taarabu
ya kawaida, baadaye katika makasri na
kumsifu Mfalme, na hata kuimba kwa
Kiarabu. Baadaye aliigeuza midundo
na mifumo ile ya kishairi na kuwa katika vinanda vya kawaida.
Matokeo yake, Taarab ya Kiswahili ilimfanya awe Nyota na yeye kuifanya
taarab iwe aina ya sanaa ambayo bado ni maarufu visiwani na isiyokosekana katika
harusi na sherehe zote za Kizanzibari ..
BARGHASH
BIN SAID
Huyu
ni Mfalme wa Tatu wa Zanzibar, aliyetawala kuanzia mwaka 1870 mpaka 1888.
Mama yake alikuwa mtumwa (aliyewachwa huru kwa kuzaliwa yeye), Sultani
wengi wa Zanzibar walikuwa watoto wa wanawake watumwa.
Baba yake, Seyyid Said bin Sultan, alikuwa mfalme mlowezi wa Sultan wa
mwanzo wa Zanzibar. Barghash
anasifika kwa ujenzi wa miundo mbinu ya Mji Mkongwe, ikiwemo maji ya bomba,
vituo vya polisi, barabara, bustani, hospitali na majumba mengi ya kiutawala
kama vile Beit el Ajaib.
Pengine alikuwa Sultan
wa mwisho kuweka kipimo cha uhuru wa kweli dhidi ya udhibiti wa Wazungu.
Alishauriana na "Washauri" kadhaa wa kizungu ambao walikuwa
na ushawishi mkubwa, lakini alibaki kuwa mtu imara waliyepambana naye
kumdhibiti alipambana na wanadiplomasia kutoka
Uingereza, America, Ujerumani, Ufaransa na Ureno na mara kwa mara aliweza
kuiangusha kitaalau nchi moja baada ya nyengine katika kinyang'anyiro cha kabla
ya Ukoloni. Ni mtoto wake, Khalid,
ambaye katika mchuano wa kurithi ufalme, alishindwa katika
Vita vifupi kabisa katika histora.
SHEIKH ABDALLA SALEH
FARSY
Alikuwa
ni mfano wa karne ya Ishirini, katika safu ndefu ya Ulamaa wa Kiislam kutoka
Zanzibar. Mchango wake maarufu
katika uislamu ni kuchapisha QUR'AN TAKATIFU, yenye kurasa 807, ambayo ni
tafsiri ya mwanzo kamili inayokubalika katika lugha ya Kiswahili
Sheikh Abdulla Saleh Farsy vile vile alikuwa kabobea katika sarufi ya
Kiarabu. Akiwa katika umri wa miaka ya ishirini, alikuwa anaandika
mashairi kwa kiarabu, jambo linaashiria ukubwa wa kiwango cha elimu ambacho
ulamaa wa Zanzibar walikuwa
wanasambaza nyakati zile.
Sheikh Abdulla aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa shule za
msingi za Unguja na Pemba mnamo mwaka 1949, Mkuu wa Shule ya Lugha ya Kiarabu
mwaka 1957 na Kadhi Mkuu wa Zanzibar mwak 1960. Aliondoka visiwani baada ya Mapinduzi ya 1964 na akafia Omani
Novemba 9 mwaka 1982.
TARIA TOPAN
Mfanya
biashara, "mwana mfalme" wa kihafidhina, ambaye alijipatia utajiri wa
mailioni kutokana na biashara ya karafuu na mamilioni
mengine zaidi wakati alipokuwa anafanyakazi kama mkusanyaji Ushuru wa
Forodha katika bandari ya Unguja na Pemba.
Katika dhamana ile, alitakiwa kumlipa Sultani kiwango kikubwa
kisichobadilika cha ada kila mwisho wa mwaka, kutokana na fursa aliyopata kwa
kuteuliwa mkusanyaji mapato. Alipiga
mahesabu na kuona kuwa angeliweza kukusanya pesa nyingi zaidi kuliko zile ambazo
angelilipa, kama ikiwa biashara ingekwenda vyema.
Na kwa wakati ule, biashara Zanzibar ilikuwa nzuri.
Bei ya karafuu na viungo vyengine ilikuwa juu, mahitaji yalikuwa makubwa na bidhaa za viwandani ambayo vitu hivi
zilifanyiwa biashara zilionyesha kushuka kupungua kila mwaka, kwa vile vitendea
kazi na mbinu za kutendea kazi vilikuwa rahisi katika nchi za Magharibi.
Kwa utajiri wake huu, Topan aligeuka kuwa mfadhili Mkuu wa
mji. Aliweka Wakfu na kujenga Kituo
cha Afya kilichonakishiwa ambacho kipo Kaskazini kabisa mwa Bandari ya Mji
Mkongwe. Vile vile
alitoa "Wakf"
vikataa vya ardhi vilivyokusudiwa kuwanufaisha wazee wasiojiweza.
NAHODHA "SMITH
WA ZANZIBAR"
Yeye
hakuwa Mzanzibari, lakini alikuwa rafiki wa mwanzo wa Kimarekani kuja Zanzibar.
Alifanya biashara kwa mapana katika mwambao wa Afrika Mashariki kwenye
miaka ya 1800. Akiwa
mfanyabaishara kutoka Salem, Massachussets, aligundua kitu
kilichomuunganisha na wafanyabiashara wa Zanzibar ambao Utajiri wao ulitokana na
mfanya biashara mwerevu na wa kuaminika. Pamoja
na manahodha wafanya biashara hawa, alifanyanao mapatano ya bei na kuweza kuwa
marafiki haraka sana.
Wamarekani
wao waliuza nguo za pamba (Mrekani) na kununua vipusa, viungo na sandarusi
ambayo ilitumika kutengeneza vanishi kwenye viwanda vya New England.
Kwa kufanya biashara na Marekani, kuliifanya Zanzibar kuwa kituo Kikuu
cha Biashara katika maeneo haya.. Hata
kufikia mwaka 1830, katika kipindi cha miezi 18, jumla ya vyombo 32 kutoka
Amerika vilishatia nanga katika bandari ya Zanzibar.Mnamo mwaka 1836 kiwango cha
biashara baina ya nchi mbili hizi ilihakikisha kuanzishwa Balozi za Amerika za
kudumu katika Mji Mkongwe. William
Smith alisafiri "kuzunguka pembe" ya Afrika mara nyingi katika safari
ndefu za kutoka Amerika na visiwani kiasi cha kujulikana kama Smith wa Zanzibar
katika pande zote za ikweta
 |