|
Ujasiri wa ZanzibarMshangao mkubwa katika Vita Fupi
Kasri la Zanzibar 1896, (Katikati) Jengo la Harem (kushoto) na Nyumba ya Maajabu (kulia) Muhtasari:Vita katika mwaka 1896 kati ya Zanzibar na Uingereza imeandikwa kama tukio fupi la kihistoria na mara nyingi limedharauliwa na kuchukuliwa kama mchezo wa kuigiza ambao haustahili kufanyiwa utafiti wa kina. Historia ya vita hii hata hivyo inaweza kuweka wazi mafunzo ya kudumu, na udogo wake kwa kweli unaweza kuleta mtazamo kwa baadhi ya masuala makubwa yaliyopo wakati wowote vurugu za kisiasa zikitokea.
Jinsi ilivyokuwa:
Kabla ya adhuhuri tarehe 25, Agosti, 1896 Sayyid Hamid Thuwain bin Said, Sultan wa Zanzibar, Pemba, Mafia, Lamu na sehemu zote za Syidi (Ukanda wa pwani ya Bara), alikufa. Kifo chake kilianzisha mapambano mara moja kuwania kiti cha utawala miongoni mwa familia za kiZanzibari. Wakazi wa Omani, ikiwemo familia ya mtawala na familia/koo nyingine maarufu zilikuwa na historia ndefu ya kujiamulia unapofika wakati wa kuchagua mtawala mpya.
Utaratibu wa kuachiana madaraka ya kisiasa Zanzibar ambao uliigwa kutoka katika taratibu za uchaguzi za kidini uliweza kuharibiwa shughuli kubwa za umwagaji damu. Ushindani miongoni jamii zinazotawala za vyama vyenye nguvu uliweza kuwa mkali. Mwaka 1859 mfumo ulielezewa kama Warithi wote wa kiume walikuwa na haki ya kuchaguliwa kuwa watawala...ikiwezekana, na kuchaguliwa na kabila, ndio haki pekee. Sultan Barghash, alipoulizwa kuhusu taratibu za kuachiana madaraka za Zanzibar aliweka wazi kwa ufupi kwa kusema haki ya kurithi Taji la Uongozi litamwangukia mshindani yule tu mwenye Upanga Mrefu. Mshindani mwenye upanga mrefu wakati Saayid Hamid alipokufa alikuwa waziwazi
ni Khalid bin Barghash. Kijana wa miaka 29, aliungwa mkono na wengi wa viongozi
wa biashara wa palepale na wamiliki ardhi wakubwa. Alikubalika kwa waHamadi wa
asili na waTumbatu na alikuwa ni mtoto wa ukoo bora. Hata hivyo hakukubalika kwa
waingereza. Mtu wao alikuwa Hamoud bin Mohamed, mpwa wa aliyekuwa Sultan wa Oman na mtu aliyependelea zaidi maisha ya kisasa. Waingereza walimuamini angeweza kuwa rahisi zaidi kufanya naye kazi kuliko Khalid mwenye akili ya pekee ya kujitegemea. Familia za Kizanzibari hata hivyo ziliuona mwingilio huu wa waziwazi katika taratibu zao uongozi kama fujo kwa utu wao na haki zao za kimila. Khalid pia alikuwa mjukuu wa baba muasisi ya nchi, Sayyid Said. Alifaulu kuwa pamoja na koo na watu wengi. Aliweza kuaminiwa na jeshi kubwa kisiwani na kabla ya saa 10:00 jioni siku hiyo ya Jumanne alitimiza majaribio ya mwisho ya kurithi madaraka, alichukua Kasri/Ngome na kudhibiti bandari, Kikosi cha majahazi na sehemu kubwa ya mji mkuu.
Amri hiyo iliendelea hadi jioni ya Agosti tarehe 25, wanaume wa kiZanzibari katika ua wa Kasri walikuwa na saa 40 kutafakari hatima yao. Ilikuwa kupigana au kukimbia. Wangekaa? Wangeweza kweli kuendelea kusubiri tu na kukodoa macho kwa Simba wa Ubereru ambaye alikuwa anakaribia kuachiliwa dhidi yao? Majeshi:
Washikiliaji Mji/Wadhatiti
Jeshi hili, kwa mtu mmoja, lilimwendea Khalid wakati mapambano kwa ajili ya madaraka yalipoanza. Kwa ziada Khalid aliwaleta wasaidizi wapatao 300 pamoja naye waliojipanga vizuri wakati alipoitwaa ngome. Mara aliposhikilia Ngome/Kasri nayo madai ya waingereza yakajulikana, waZanzibari wengine 1,500 wakakimbilia kwake. Hii ikafanya jumla ya vikosi 2,800. Wanaume wakajipanga kulinda Kasri, Jengo la Harem lilikuwa karibu na uwanja uliokuwa mbele ya ua upande wa bahari. Jeshi la majini la Zanzibar ambalo majahazi yake ya kivita kwa muda mrefu yalikuwa yakidhibiti pwani ya Afrika Mashariki hadi muda huu yalikuwa yameuzwa au kubadilishwa kwa matumizi ya kibiashara. Jeshi la waingereza la majini lilikuwa limechukua jukumu la kutuliza ghasia katika Bahari ya Hindi. Pia ufundi stadi wa Meli ya Mvuke ya Kivita iliyokuwa imenunuliwa kama Meli ya Kibendera ya Sultan na chombo hiki H. H. S. Glasgow kilichopewa jina kufuatia mahali kilipotengenezwa, kilisimama kimetia nanga bandarini. Wafanyakazi wa meli Glasgow waliapa kiapo cha uaminifu kwa Sayyid Khalid akiwa kama Sultan wao mpya na wakafyatua mizinga ya heshima kutoka katika mizinga ya zamani lakini ya mizuri. "Serikali"
Mathews alivipa vikosi vyake mazoezi ya kutosha na vilionesha nidhamu na moyo wa kupambana wakati wa safari za mara kwa mara pwani ambazo walizifanya kwa maagizo ya serikali (na/au Mwingereza Mkazi). Pia mwanzoni walikuwa jeshi la miguu bila silaha nzito.
Wanadiplomasia hatimaye waliaamua wangejisikia salama zaidi na waliamini wangeweza kuwa na uwezo zaidi kwa vikundi hivi , kwa kuviweka katika sehemu za ulinzi, kusini ya Kasri/Ngome, kuzunguka sehemu ya diplomasia ya jiji. Jeshi la Majini La Kifalme.Zikiwa zimetia nanga bandarini wakati huo wa kifo za Sultan mwanzo zilikuwa ni meli za waingereza H.M.S. Philomel na boti ndogo ya mizinga H.M.S. Thrush. Ziliungana na meli nyenzake Thrush, H.M.S. Sparrow mnamo saa 11: 30 jioni. Baadaye siku hiyo hiyo ya Jumanne jioni majeshi ya serikali mjini yaliongezewa nguvu vikosi vya waingereza ambavyo havikutarajiwa vilivyoshuka kutoka katika meli hizi. Vikosi vya majini vilikuja na mizinga fulani ya jeshi la majini, Kwa kadirio la chini mzinga mmoja na machineguns (Maxim guns) mbili kubwa. Hizi mara moja ziliwekwa kuzunguka Ubalozi wa Uiengereza. Kisha vikosi vingine vya jeshi la majini vilianza kujikusanya. Nyingine iliyofuatia kuonekana karibia saa 3:00 asubuhi siku ya Jumatano, ilikuwa meli kubwa H.M.S. Raccoon na kisha adhuhuri mwezi Agosti tarehe 26, 1896 meli kubwa sana Flagship H.M.S. Mt. George ilitia nanga katika bandari ya Zanzibar. Kwa pamoja meli hizi tano zilibeba mizinga 78 mikubwa ya aina saba tofauti tofauti, ikianzia mizinga ya mitutu 3 hadi ya inchi 9.2. 1. Mizinga 20 ya mitutu 3 2. Mizinga 12 ya mitutu 6 3. Mizinga 8 ya mitutu 9 4. Mizinga 12 ya inchi 4 5. Mizinga 8 ya inchi 4.7 6. Mizinga 16 ya inchi 6.0 7. Mizinga 2 ya inchi 9.2 Meli hizo zilikuwa ma bunduki mashine nzito na kila moja ilkuwa na milio kadhaa na stendi ambazo rekodi za jeshi la majini zilizobebwa zingeweza kuwekwa. Meli zilisogea pembezoni ufukoni , wakizunguka karibu sana na uzio ulioimarishwa. Meli H.M.S. Sparrow ilimalizia siku ya pili ya mzozano ikatia nanga moja kwa moja mbele ya kasri/Ngome, Meli H.M.S. Thrush ilikuwa mbali kidogo kaskazini lakini karibu na ufukwe wa bahari, yadi 200 tu kutoka ukingo/ukuta wa bahari. Kwa kweli hili lilikuwa jeshi kubwa sana la kutisha lililowahi kujikusanya wakati huo katika Afrika Mashariki. Nyakati zenyewe hasa:Hatua ya Zanzibar kwa huu mkusanyiko wa majeshi ilikuwa kuendeleza mapambano kwa upande mmoja na jitihada za kidiplomasia kwa upande mwingine. Uingereza ilitoa waraka wa maandishi wa mwisho. Sultan Khalid aliambiwa kwamba lazima aichie Ngome na atawanyike na majeshi yake au la sivyo uingereza imshambulie. Alishauriwa zaidi na uingereza British kuwa "kuwa ameushikilia Usultani wa Zanzibar bila ya kupata ushauri wao " alikuwa "ametenda kitendo cha uasi dhidi ya serikali yake malkia tukufu ya Uingereza." Uingereza walikataa kuzungumza na wasingewasiliana zaidi na majeshi ya waasi Sayyid Khalid alijibu kuwa hatashambulia wazungu na alichotaka ni amani tu kati yao. Pia alisema kuwa asingeweza kuicha ngome/kasri, " nyumba yake na nyumba ya baba yake". Aliwasiliana na serikali za Ufaransa, Marekani na Ujerumani kutafuta kupata kauli yao. Wote walikataa; Nchi hizi zote zilkuwa na na makubaliano ya mkataba na Uingereza kwamba kwa njia moja au nyingine kutojihusisha na lolote kwa Uingereza kuhusu masuala yote ndani ya makoloni yao. Sultan alimuomba balozi wa Marekani kutoa taarifa kwa Malkia wa Uingereza. Taarifa ilisomeka: " Malkia Victoria, London. Hamed bin Thweni amefariki. Nimefanikiwa kuchukua kiti cha madaraka mababu zangu. Natumaini mahusiano ya kirafiki yataendelea kama mwanzo. Khalid bin Barghash, Sultan." Taarifa hii haikuwahi kufikishwa/kupelekwa. Baadhi wametoa maoni kwamba jitihada zote hizi za kujiingiza katika biashara ya umbali mrefu (bila shaka ndefu hasa) kampeni za kidiplomasia zinaonesha kuwa waZanzibari hawakufahamu hatari ya mara moja na walikuwa wajinga kutotambua jinsi gani silaha za Uingereza zilivyokuwa za hatari na jinsi gani jeshi la majini lilivyokuwa tayari kuzitumia. Dhana hii sio sahihi. Hakuna shaka kwamba uongozi wa Zanzibar ulijua kwa undani jinsi gani majeshi ya waingereza yalivyoweza kuwa ya hatari kubwa. Tangu zamani kabisa enzi za utawala wa mababu zake baadhi ya mawaziri wa Khalid's walisafiri Ulaya na walitembelea viwanda vikubwa vya silaha vya mapinduzi makubwa ya uundaji. Walikuwa miongoni mwao pia na miaka ya uzoefu wa utengenezaji mizinga ya jeshi la majini na walikuwa wameona kwa macho yao shughuli za jeshi la uingereza hivi karibuni katika bahari ya Hindi kwa makini hasa.
Alexandria ulikuwa ni mji iliokuwa maarufu kwa harakati za utaifa za Misri na kituo cha upinzani kwa serikali kibaraka iliyowekwa madarakani na Uingereza. Wakati wanaharakati wa utaifa waliposhika udhibiti wa jiji meli kumi na tisa za waingereza ziliwashambulia. Utayari/Nia ya meli za waingereza kushambulia katika miji yenye wakazi wengi haikuwa tena mashakani katika sehemu hii ya dunia. WaZanzibari walijua kikamilifu kitachogharimu msimamo wao kuendelea kupinga, lakini bado walisubiri. Hakuna hata mtu mmoja aliyeondoka na kuiacha Ngome ile iliyoimarishwa. Usiku ulipoingia Khalid alitoka kwenda kwenye msikiti wa jamii kusali na kuonesha alikuwa haogopi kutembelea mitaa. Na mara usiku ulipozidi kimya cha kutisha kilitanda juu ya jiji. Baadhi ya mashahidi/waliokuwepo walisema kwamba "hawajawahi kuona usiku mkimya wa namna hiyo". Mwingine aliandika kuwa "Ukimya ulikuwa mkubwa na wa kutisha .....Kelele za hatua za miguu na sauti za kutafunatafuna na kuongeaongea zilizofanywa na maelfu ya binadamu wakati wakila, fanya kazi, cheza na kuzunguka zunguka: zote hizi zilitulia/nyamaza, na wakati huo mji ulikuwa umejaa hofu na wasiwasi." Mapigano:
Maoni ya Marekani yalikwisha julikana kwa kazi hii ya suluhu iliyofanywa na Zanzibar kwa sababu USA haikuwa mojawapo ya mataifa "yaliyopewa" sehemu ya Afrika katika mkutano usio wa kinyama wa Berlin wa mwaka 1885. Vilevile wahusika wakuu wa Marekani walikataa kupeleka taarifa au katika njia yoyote kuhoji haki ya "Taifa lenye nguvu" kuwapeleka watu wa nchi hiyo katika kifo. Hii hasa ilikuwa siku mbaya sana kwa harakati za kidiplomasia Agizo/Tamko la mwisho la waingereza iliweka saa 3:00 asubuhi kama muda rasmi kwa vita kuanza, Majeshi ya Majini yangeshambulia ikiwa majeshi katika Ngome/Kasri yasingesalimu amri hadi wakati huo. Kabla ya saa yenyewe kuwadia tukio la kijasiri lilitokea. Boti ndogo iliondoka katika uzio wa Zanzibar na kusogea taratibu ikapita meli tatu za Uingereza. Mpango wake ulikuwa kumpeleka nahodha wa Sultan katika meli yake pekee H.H.S. Glasgow. Meli hiyo ya kivita ya mbao ilizungukwa na kubwa 5 zenye ngao lakini men watu waliokuwa ndani yake hawakuhangaika kutia nanga wala kukimbia. Nahodha alipofika kwa nguvu walianza matayarisho ya mwisho yaliyohitajika kufyatua mizinga yao ya zamani na wakazilenga meli mbili za Uingereza zilizokuwa karibu. Waingereza waliona kitendo hiki ni cha ukaidi na kwamba hakuna bendera iliyoshushwa na Zanzibari asubuhi hiyo. Kikosi cha meli cha Uingereza kilishambua kwanza, kwa usahihi kwa wakati huo na moja kwa moja kwa wanaume wa kiZanzibari waliojikusanya ufukoni, Zanzibari mara moja wakajibu mashambulizi. Mnamo saa 3:05, pamoja na sehemu yake ngumu, meli H.H.S. Glasgow ilimfyatulia adui. Kisha waingereza wakaelekeza mashambulizi mazito tokea pande zote mbili kwenye meli Glasgow. Ikiwa imetobolewatobolewa karibu na mkondo wa maji mara moja ilianza kuzamishwa kwa kasi, huku ikifyatua muda wote ilipokuwa ikienda chini ya maji. Watazamaji walizikimbia paa wakati maganda yaliyorukaruka ovyo yalipopitiliza na kutua juu ya uzio kabambe, yakiwasha moto sehemu kadhaa ndani ya jiji. Watazamaji wale waliobaki juu waliweza, kwa muda mfupi, kuona moshi kutoka tika mizinga katika pande zote mbili zikishambulia lakini muda si mrefu moshi zaidi kutoka katika moto wa milipuko, ulifunika uzio wa Ngome/Kasri usiweze kuonekana. Bado meli za waingereza ziliendelea kushambulia. Imekadiriwa kuwa karibu ya maganda/mizinga elfu moja ilifyatuliwa Zanzibar siku hiyo. Ikiwa ni kweli basi hiyo ina maana ganda lilianguka kwa kila baada ya sekunde tatu kwa saa hiyo ya mashambulizi. Kwa sababu ya maoni potofu maelezo mengi yanaangalia zaidi uzito wa mapigano badala ya mafunzo yake. Shahidi mmoja atuambia kuwa "Kwa dakika arobaini na tano kelele za kuogofya/ogopesha ziliendelea: miungurumo ya kuudhi, iliyofutiwa na michakacho ya maxims (bunduki mashine) na mlio wa mtutu mmoja, maganda yakilia hewani na vipandevipande vyake vikidondoka hapa na pale ovyoovyo." Kabla ya saa 3:30 asubuhi Meli Glasgow jasiri ilikuwa kimya, mizinga yote iliharibiwa na idadi kubwa ya waliokuwemo walikufa ama kujeruhiwa. Meli taratibu ilizama kwenye kina kifupi cha kichanga cha bahari, milingoti yake bado inaonekana juu ya maji. Mashambulizi kutoka kwa wazanzibari ufukweni yalipungua, na bunduki zao za zamani moja baada ya nyingine zilichukuliwa. Mashambulizi ya waingereza pia yalionekana kupungua wakati wafyatuaji waliposhindwa kuona shabaha katika moshi na maafisa walianza kuangalia kama kuna dalili/ishara za kusalimu amri. Ndani ya uzio liliweza kuonekana jengo la Harem lililokuwa likiungua kwa moto mkali kwa kuwa kulikuwa na mabohari karibu na maji. Kisha upepo uliupuliza moshi upande na hivyo kuruhusu muonekano mkubwa wa wahusika wakuu wenye bendera wa Ngome/Kasri; wakiwa na bendera ya rangi nyekundu ya Zanzibar bado ikipepea. Waingereza walirudia tena mashambulizi yao kwa nguvu zaidi na tena mandhari punde tu ilifunikwa na moshi.
Aina fulani ya maelezo ya kutunga ya ya tukio hili la mwisho yalitolewa na mwingereza akiandika mwaka mmoja tu baada ya vita hiyo.
"Kwa kutokea nyuma kila moja ikilinda boti jasiri/bishi zilizojaa zikilenga ...lakini kuingia kwa vikosi vyenye majaketi ya bluu hakuwi hivihivi tu bila mapambano na upande mwingine wa pili. Hapa na pale milio ya mizinga na bunduki, na kwa wakti huohuo idadi kubwa ya risasi zikidumbukia bila madhara katika maji ya bluu ya bahari ya bandari, na chache zikipata nafasi miongoni mwa waliokuwepo katika boti." Matokeo: Wakiwa bunduki zao zote lakini zilizoharibiwa na vikosi vya majeshi ya maajini vya Uingereza wakija ufukweni kwa mamia, Khalid mara ya mwisho aliwapa amri ya kuondoka katika uwanja wa mapambano. Wakiacha watu 500 wamekufa ndani na kribu ya ya Ngome, Sultan huyo aliwahimiza wanamgambo wa wakiZanzibari kuwachukua waliojeruhiwa na kurudi nao nyuma ya jiji walipotokea. Kisha akawaongoza watu wake waliobaki wakiwemo walinzi wa ngome, katika matembezi ya hatari kupita jiji kulekea katika Ubalozi Ujerumani. (na kuelekea katika majeshi ya kujitolea ambayo yalikuwa bado hayajaruhusiwa kuondoka katika maeneo yao ya ulinzi.) Shahidi mmoja ambaye alikuwa karibu na uwanja wa diplomasia aelezea tukio hili: "Kilichokuwa cha kushangaza kwangu niliwapofikia wawakilishi kuona idadi kubwa ya waarabu na wafuasi wao, wakiongozwa na Khalid, wote walijaa vumbi na damu, wakija upande wangu na kuelekea katika Ubalozi wa Ujerumani." Khalid alielekea njia yake akipita kundi moja la majeshi ya waingereza, ambayo hayakumtambua, na alifikia sehemu maalum ya kufanyia mazungumzo. Wajerumani pale walikuwa na sababu zao za kusaidia mpinzani wa waingereza na walimkaribisha na idadi ndogo ya wasindikizaji wakuu. Wanajeshi wake mara walichukuliwa silaha zao (na silaha zao ziliharibiwa) lakini baada ya hapo waliweza kuelekea na kupotelea ndani ya kisiwa wakati majeshi ya serikali na vikosi vya uingereza vilitakiwa kudhibiti mapigano ambayo yalitishia kuugubika mji na pia kushughulika na ghasia zilizotokea mara matokeo ya vita yalipojulikana.
"Mzinga wa inchi 6 wa kufyatua haraka kwenye meli ya Kifalme ya Arthur, meli nyenzake St. George (Meli ya kubeba Bendera ya waingereza wakati wa vita ya Zanzibar)... ina rekodi ya kumi na nane ya zilizolengwa katika muda wa dakika tatu. Ikiwa kiwango hiki cha mashambulizi ya mapigo sita kwa dakika ingeendelezwa kwa dakika thelathini na saba (muda uliofikiriwa wa vita )... mzinga mmoja wa haraka ungerusha mizinga 222, ikiwa na uzito wa paundi 100 kwa kila mzinga kulekea jijini. Meli ya St. George inabeba mizinga ya namna hiyo 5 kwenye sehemu yake pana...Pia iliweza kuleta (kwa wakati huo) mizinga fulani mikubwa 120, ikiwa na uzito wa paundi 320 kwa kila moja, kutoka katika mizinga yake ya inchi 9.2.
Alamo barani Afrika![]() Imesemekana vita hiyo fupi kabisa ilifanana na Mapinduzi ya Marekani ya mwaka 1776. Katika vita vyote wapiganaji walipinga haki ya Himaya ya waingereza kutawala bila kuruhusu udhibiti mzuri wa kutosha wa mifumo ya jamii na uchumi wa wazawa. Vilevile vita ya mwaka 1896 kati ya waingereza waZanzibari, ikiwa ya pambano moja, labda ni vizuri zaidi kuifananisha na vita maarufu ya wamarekani katika Alamo. Katika vita zote mbili, maelezo ya mapambano yamekuwa muhimu zaidi kuliko matokeo ya mbinu zilizotumika. Kwa hali hiyo kikundi kidogo cha wapiganaji wa Texas walichukua sehemu muhimu zilizolindwa na walizitamisha chini rundo la bunduki za Jeshi lenye nguvu la wamexico army bila kurudi nyuma. Kwa sababu ya kuzingatia kwao kanuni za kujitegemea pamoja na kujiamini waliibuka washindi/mashujaa wa taifa. Katika vita ya mwaka 1896 kikundi cha wapiganaji wa Zanzibari walizitazamisha chini rundo la bunduki la majeshi ya waingereza na wengi wao walikufa kuliko kukata tamaa katika nia yao. Hiyo ni simulizi ambayo haipaswi kusahauliwa. Mfano wao pia ni funzo wa kutafakari hata leo, wakati waZanzibari wapigana na waZanzibari na majeshi yenye nguvu ya taifa na kimaitaifa yakishindana kutawala eneo. Bila kufuatilia kwa makini/kwa karibu vilio hivi vya watu wa visiwa hivi tutaona Alamo nyingine barani Africa?
Ifuatayo hivi karibuni:Zanzibar na Vita Kuu: 1914-16
Bonyeza hapa upate Vyanzo na Maelekezo. Sources and Bibliography Webmaster: Barghash@msn.com
Imetengenezwa mwaka 2002, kwa ajili ya Firdawsi na Mohammed. Haki Zote Zimehifadhiwa. Imetafsiriwa na Mwalimu George Mwidima gmwidima@yahoo.com |