Kupiga mbizi zanzibar
Maji ya
Bahari ya Azania yanachangia katika kupatikana kwa maarifa mazuri ya kuogelea,
kupiga mbizi na kuzamia duniani. Yapo makampuni
mengi katika mji mkongwe yanayojishughulisha na upigaji mbizi na baadhi
yako katika fukwe ndefu za kitalii. Zote hizi hutoa huduma za upigaji mbizi na
zinaweza kutayarisha safari za kupiga mbizi katika miamba ya karibuni na katika
visiwa vidogo vidogo. Kituo cha Taifa cha mambo ya Baharini kilifunguliwa
karibuni huko kisiwa cha Chumbe, maili 12 tu kusini Magharibi mwa mji mkongwe.
Huko kuna miamba ya matumbawe mizuri na aina mbali mbali za viumbe vya
kushangaza vya baharini na pia fursa ya kupiga mbizi na kuzamia hupatikana
sambamba. Boti za kukodi vile vile huondoka mji mkongwe kuwapeleka wapiga mbizi
katika kisiwa cha Pemba. Huko utaweza kuona kwa macho yako wakati unapiga mbizi
katika maji meupe ya
uvuguvugu (maji ambayo jicho linaweza kuona chini kati ya futi 60 hadi 2000),
nje ya Kisiwa cha Mesali, ambako utaweza kupata maana halisi ya msemo "furaha
ya kina".
Ifuatayo hapa ni orodha ya baadhi tu ya visiwa vidogo
vidogo, miamba, fungu za mchanga na visiwa vya matumbawe vinavyofaa kwa kupiga
mbizi kote Unguja na Pemba. Hadhi au daraja za uzuri wa sehemu hizo zimo katika
kitabu kipya (1997) cha Anton Koornhof kiitwacho "Maeneo ya kupiga mbizi
Kenya na Tanzania" (kilichochapishwa na
Passport Books, Chicago 111 USA).
Maeneo ya Kupiga Mbizi Karibu
Mji Mkongwe
Kisiwa cha Changuu
(Prison Island) ni kizuri kwa kuzamia kwa kutumia vifaa vya hewa. Ni sehemu
iliyo mita 35 tu Kaskazini Magharibi ya ufukwe.
Kisiwa cha Chapwani (Grave
Island) = Ni kizuri pia kwa kuzamia, mita 50 Kaskazini Magharibi kwenye ncha ya
Kaskazini ya kisiwa.
Kisiwa cha Bawe:
Koornhof amekipa hadhi ya 4
kwa kupiga mbizi na kwa kuzamia.
Ukuta wa mwamba upo umbali wa mita kama 150 Kaskazini mwa ncha ya Kaskazini ya
kisiwa.
Fungu
Chawamba (Sand Bar) = kipo umbali wa kilomita 3 Magharibi ya mji mkongwe.
Kampuni nyingi za upigaji mbizi za mjji mkongwe hulitumia fungu hili kwa wale
wanaoanza kuogelea kwa kutumia chupa za hewa.
Nyange (eneo
ambalo halikuwekwa maboya) Koornhof amelipa sehemu hii hadhi ya kwanza
kupiga mbizi na kwa kuzamia.
Kisiwa cha Pange
- Kornhof ameipa sehemu hii hadhi ya kupiga
mbizi na kuzamia.
Kisiwa cha Pwaku
= Koornhof ameipa sehemuhii hadhi ya
kupiga mbizi na kuzamia.
Kisiwa cha Murogo:
Koornhof anakipa kisiwa hiki hadhi ya
kupiga mbizi na kwa kuzamia.
Fungu mchanga la
Boribu (vile vile linaitwa Bokibu) Koornhof analipa hadhi ya kupiga
kupiga mbizi na kwa kuzamia.
Kisiwa cha Chumbe:
Kibali kinahitajika kwa wale wanaokwenda kupiga mbizi kwenye hifadhi ya
Maisha ya Baharini lakini pesa zinazotozwa ni muafaka na kinatilia mkazo mwamko
wa mazingira. Katika kisiwa hiki upo mnara maarufu.
Maeneo mengine ya kupiga mbizi Unguja
Stringray Alley:
hutumika kwa kupiga mbizi na haifai kuzamia. Sehemu hii ipo mwambao wa
Mashariki ya Unguja, Mashariki ya Shehe Guest House,
karibu na kijiji cha Jambiani.
Mwamba wa Jambiani:
(vile vile panaitwa Mwamba wa Pembe moja) Hutumika kwa
Kupiga mbizi na hapafai kwa kuzamia. Upo dakika 30 tu
Mashariki ya kijiji cha Jambiani kwa kutumia mitumbwi ya kienyeji.
Levan
Bank: Hutumika kwa kupiga
mbizi na hapafai kwa kuzamia. Sehemu hii ipo nje ya kijiji cha Nungwi, kwenye
ncha ya Kaskazini mwa kisiwa kikuu.
Kisiwa
cha Mnemba Hutumika kwa
kupiga mbizi na kuzamia. Hiki
ni "kisiwa binafsi " nje ya mwambao wa Kaskazini Mashariki.
Maeneo
ya Kupiga Mbizi Pemba.
Kisiwa
cha Mesali: Kisiwa hiki kinanipendeza
binafsi! Vile vile kinaitwa kisiwa cha Nahodha Kidd na kinaaminiwa kuwa bado
kuna hazina yake iliyofukiwa . Kipo upande wa Magharibi ya mji wa Chake chake.
Hadhi yake ni kupiga mbizi na
kuzamia. Kinastahiki kabisa hadhi hiyo.
Kipengo
cha Uvinje: Zipo sehemu mbili za kupiga
mbizi katika sehemu hii ya Kaskazini Mashariki ya
Chake. "Ukuta wa Kaskazini" umepewa hadhi ya kupiga mbizi lakini hapafai kuzamia, wakati "Ukuta wa
Kusini" una hadhi ya kupiga
mbizi na kuzamia.
Kisiwa
Panza: Kipo
karibu na ncha ya Kusini ya kisiwa cha Pemba. Sehemu hii ina maeneo mawili pia.
Eneo la kwanza linaitwa "meli ya kusini," karibu na meli ya mizigo
iliyozama, ambapo pana hadhi ya kupiga
mbizi na hapafai kwa kuzamia. Kusini kwa meli hiyo iliyozama upo "mwamba wa
zumadiri penye hadhi ya kupiga
mbizi na pia hapafai kwa kuzamia.
Ncha ya Taa:
Hii ipo nje ya mwambao wa Kaskazini Magharibi ya Pemba,
karibuna kisiwa cha Fundo.
Hapa pana hadhi ya
lakini hapafai kuzamia. Sehemu hii inajulikana hivyo kwa sababu ya idadi
kubwa sana ya taa, wakubwa wa taa ufukweni mwa kisiwa cha Pemba mara nyengine
hutumika kama eneo ka kupiga kambi kwa vikundi vya wapiga
mbizi.

Anuani kwa Wapiga Mbizi
One
Ocean Zanzibar
Diving Centre: Moja ya kampuni nzuri ya wapiga mbizi
zanzibar na kupiga mbizi popote kwa kutumia madau.
http://www.webworks.com.
au/zanzibar/zdcmain.htm
Dive Africa Water
Sports : imeunganishwa na ramani ya mawasiliano ya upigaji mbizi kaskazini
ya unguja.
http://www.diveafrica.com/zanzibar/index.html
Rising
SUN dive Centre : kampuni
ya kupiga mbizi mwambao wa mashariki.
http://www.risingsun-zanzibar.com/main.html
Bondei
Travel : Utaratibu wa
biashara ya kupiga mbizi na orodha ya bei.
http://www.bondei-travel.dk/DIVING.htm#Mafia%20Island
UV-bilder frn
Zanzibar-1998 =Kuna picha nyingi nzuri za ndani ya maji.
http://www.eminds.se/ka/uv/Zanzibar-1998/
New Africa Com =
Ramani nzuri iliyounganishwa na mawasiliano ya upigaji mbizi katika kisiwa
Mafia.
http://www.newafrica.com/travel/mafia/
New Africa.com
= kisiwa chengine kizuri cha kupiga mbizi katika kisiwa cha Pemba
http://www.newafrica.com/travel/pemba/
Chumbe Isle Home page
= Kupiga mbizi katika
hifadhi za matumbawe
http://www.xtra-micro.com/work/chumbe
Habari
nyengine kwa wapiga mbizi.
Joto la maji katika sehemu zote ni kati ya nyuzi joto 25
hadi 29 kwa kipimo cha senti grade.
Hali ya usafi wa bahari mtu anaweza kuona chini ya maji
kati ya mita 15 - 60. Kwa kawaida ni vizuri kwa wapiga mbizi kufanya hivyo
wakati maji yanapoaanza kujaa, kwani wakati wa maji kupwa kunaweza kutibua
bahari na kumfanya mtu asione chini.
"Msimu wa kupiga Mbizi" kuanzia Septemba hadi
Machi lakini ukweli ni kuwa maeneo mazuri ya kupiga mbizi yapo kwa kipindi chote
cha mwaka. Ni kinyume na sheria kwa wapiga mbizi kuvua kwa kutumia bunduki
ingawaje wenyeji wamekuwa wakifanya hivo kama kawaida . Sehemu ya karibu za huduma za kupiga mbizi ipo
Mombasa Kenya kwenye kituo cha wanamaji.
Kupiga Mbizi Usiku .
Kama unataka msisimko wa aina yake jaribu kupiga mbizi
usiku katika moja ya maeneo ya yenye maji ya kina kifupi toka orodha ya sehemu
zilizotajwa. Maji safi pamoja na kundi kubwa la viumbe vya baharini vyenye kutoa
mwanga hufanya mandhari yaonekane ya kusisimua sana. Mara moja nilikuwa
ninazaniwa kando ya kisiwa cha changuu wakati wa mwezi mpevu na niliyoyaona hapo
hayawezi kusahaulika na katika usiku wa giza na kama utabahatika kupata maji
muafaka unaweza kuona naonesho hata bila ya kuigia majini. Adrian Conan Doyle
alitumia sehemu ya malipo ya babu yake ya uandishi vitabu kwa kuja kwenye maji
ya aina hiyo katika m,iaka ya 1950. Haya hapa ni maelezo yake ya usiku
mmoja alipokuwa ametia nanga katika dimbwi la maji lililotenganishwa na
fungu, kusini mwa kisiwa cha Unguja.
"Taa za Mauti"
Huku tukiwa tuko kimya kabisa, tulisimama kuangalia.
Ilielekea kuwa kulikuwa na anga kubwa la mwangaza lililotokea chini kabisa ya
bahari, na kadiri lilivyokuwa linakaribia, liliifanya sehemu yote ya chini ya
meli, mle mlimofikia maji, kuanzia kung'ara . Mwanga ule unapita moja kwa moja
chini ya mkuku wa meli, wakati mimi nikiwa deki nimeshikilia chubwi ya risasi,
nikairembea majini. Ghafla kundi lote lile likatawanyika na kugeuka ndimi moto
wa kibuluu zinazofukuzana mithili ya vimondo gizani ndani ya maji. Lilikuwa
kundi la samaki wakubwa. Kule! Alipiga kelele Anna. Na kule vile vile! Oh!
Yalikuwa mandhari mzuri kabisa. Makundi ya samaki yalianza kutembea kama
mkondo kutoka ndani ya dimbwi lile; huku wakitoa mwangaza hafifu kutoka
umbali wa yadi mia moja, hivi, na taratibu wakawa wameunda vikundi vizuri vya
rangi za buluu na kijani kuelekea baharini. Kwa kuwaangalia kwa makini sana ,
mtu aliweza kumaizi kuomba anga zile za mwangaza uliokuwa unatembea
zilisababishwa na kundi zima la samaki wa ukubwa wa kadiri.
Saa zilipita na baada ya muda mrefu Anna aliondoka kwenda
kupumzika. Makundi yale ya samaki yaliyokuwa yanatembea sasa yalikwishapungua
sana nami nilikuwa tayari kuteremka wakati ghafla, nyuma ya Omo, lilichomoza
anga jengine la mwangaza kwa mbali chini ya bahari. Lilikuwa linakuja karibu
karibu zaidi na sasa nikawa naweza kuhesabu si zaidi ya makundi matatu
yaliyofuatana moja nyuma ya jengine katika mstari mmoja mkubwa, huku yanatoa
mwangaza wa kijani.
Samaki wale wakapita sambamba na meli, huku muundo sawa na
umbo la almasi ukitoa mwangaza wa buluu, na mapezi yao yakiwa na ukubwa wa zaidi
ya futi thalathini kutoka ncha hadi ncha. Walikuwa
wakielekea gizani na kuwacha mkondo wa mwangaza usio na moto utadhani
mahema makubwa yaliyokuwa yakiserereka. Hivyo ndiyo taa hao walivyokuwa wanapita.
Na Barghash 2001 Barghash@msn.com
 |