Historic Photographers
Zanzibar Sketches
Palatial Zanzibar
Zanzibar mosques
Zanzibar Women
Kanga and Zanzibar
Six Famous Zanzibari
Oman and Zanzibar
Zanzibar Courage
Goa and Zanzibar
Zanzibar Christians
Zanzibar Ships
Lights of Zanzibar
Tumekuja School
Zanzibar Golf
Space Station Zanzibar
A Funeral In Zanzibar
Zanzibar Fire
Zanzibar Revolution
Nine Hour Revolution
Mass Graves
Images of a Revolution
??? ?????? ?? ???????
KiSwahili Pages
Diving Zanzibar
111 Links
Table of Contents
Search My Site
GUESTBOOK

Zanzibar Yetu

Unguja na Pemba, Tumbatu na Mafia.

"Visiwa vilivyojitandaza kama kito katika upwa wa Afrika"

Visiwa vikuu vya Zanzibar ni Unguja na Pemba, Tumbatu na Mafia. Mji Mkongwe ulio katika ufukwe wa Magharibi ya kisiwa cha Unguja, ndio mji mkuu wa eneo hili. Kwa hakika hasa, maeneo haya yamejengwa kwa miamba na chokaa, sio mawe. Kwa sasa, kuna takriban majengo 1700 ya aina hii katika sehemu ya mji mkongwe wa Zanzibar. Kati ya haya , 1100 yametambuliwa kama majengo yenye thamani kubwa katika utaalamu wa ujenzi. Katika eneo hili dogo, ambalo asili yake hasa kilikuwa kipande cha ardhi kilichozungukwa na bahari mithali ya kisiwa kidogo, na ambalo ni kiasi cha eneo liingialo majengo 83 kwa vipimo vya mji, kuna chochoro 23, makanisa 2, zaidi ya misikiti 50, Roshani 50, varandaa na baraza na zaidi ya milango 200 iliyonakishiwa kistadi. Mji mkongwe wa Zanzibar umechaguliwa kuwa "Eneo la urithi wa Kilimwengu" na Umoja wa Mataifa.

Umri hasa wa mji mkongwe haufahamiki. Je, uliibuka kutokana na kijiji cha wavuvi kilichojulikana kuwepo katika kipande kihi cha ardhi tokea karne ya 12, au mji huu ni mkongwe zaidi? Je, mji huu ni matokeo ya uhamiaji wa karne ya 10 kutoka Uajeni" Au ni matokeo ya safari za karne ya 9 za Maulamaa wa Kiislamu" Au makazi ya karne ya 1 ya Malkia Bilqis wa Shaba? Mambo yote haya yanapendekezwa na wanahistoria kuwa yaweza kuwa tarehe ya kuanza kwa mji huu. Ama twapaswa kuangalia nyuma zaidi, kiasi ya miaka 5000 hado 6000 iliyopita, pale wakaazi wa ndani ya Bara la Afrika walipovuka bonde la ufa na kuanza kuvikalia visiwa vya Afrika Mashariki. Ni wao kweli walioanzisha ustaarabu wa Madola ya mji ya visiwa kutoka lamu hadi Lindi? Je, ni kweli kuwa visiwa hivi vya mji mkongwe vina mawanda ya takribani kilomita 1000?

Likiwa eneo kubwa kuliko yote la mji mkongwe ya waswahili, Zanzibar ni sehemu bora kutembelea. Watalii sasa wanakaribishwa na huduma za kitalii zimekuwa zikitanuliwa zaidi tokea miaka michache iliyopita. Hoteli na nyumba za kulala wageni zinapatikana kwa bei unayoimudu. Kuna malazi kuanzia ya gharama ndogo hadi yale ya kifahari. Uwanja wa ndege wa kimataifa upo kilomita 5 tu kutoka mji mkongwe wenyewe na vyombo vingi vya kisasa, vya baharini sasa hufanya safari kwa muda mchache tu baina ya visiwani na Bara. Kwa wale wasiomudu kusafiri kwa sasa, basi nawafaidike kwa picha, vidokezo na habari kuhusu Zanzibar, kihistoria na watu wake.


Home Wazanzibarr_Maarufu.htm WAPIGA PICHA WA KIHISTORIA WA ZANZIBAR Zanzibar Maridhawa Michoro ya Kale ya Zanzibar WANAWAKE WA ZANZIBAR Ujasiri wa Zanzibar Misikiti ya Zanzibar Oman na Zanzibar WAGOA_na_zanzibar WAKRISTO WA ZANZIBAR Sherehe ya Miaka 25 ya mwaka 193 KITUO CHA ANGA ZANZIBAR SKULI YA TUMEKUJA Mazishi Zanzibar Kupiga mbizi Zanzibar Tovuti mia moja kumi na moja za Zanzibar MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAPINDUZI YA SAA TISA MAKABURI YA HALAIKI

Webmaster: Barghash@msn.com

Hit Counter