Kuendesha Chetezo kwa Upepo Zanzibar

Wakati wa pepo za masika, kwenye mkondomaji wa Zanzibar, vifaa vyote vieleavyo vya kila aina viliweza kufikia/kwenda kasi kubwa. Picha hii baadaye ilitengenezwa stempu. Mtu ni lazima ashangae jinsi gani hasa picha hii ilivyochukuliwa/pigwa.

Taxi Maji

Kwa miaka mingi Mji Mkongwe karibu wote ulizungukwa na mikondo ya maji. Watu bado waligundua njia/namna za kutoka, kwenye hayo maji yaliyojaa au kupwa.

Wanamuziki 1900

Muziki na ngoma sikuzote zimekuwa sehemu ya utamaduni wa Zanzibar.

Gereza

Matanga ya majahazi ya zamani yaliungwaungwa pamoja na kukaa imara na yalikuwa katika hali ya kukarabatiwa karibu mara kwa mara.

Mashua ya Sultan

Mashua hii ya Taifa ilitumiwa mara kwa mara kumtoa Sultan nje ili kutembelea meli bandarini. Angeweza pia kuiagiza kwenda kivukoni kwa wageni muhimu watakao kumuona.

Gereza

Mizinga mbele ya Jela yaonesha kuwa picha hii ilichukuliwa punde tu baada ya Vita ya 1 ya Dunia.

Jengo la Mawasiliano la Mashariki

Kutoka katika sehemu hii ya kawaida waya nyingi za chini ya maji ziliunganishwa. Hii ilikuwa sehemu muhimu ya mtandao wa zamani wa mawasiliano duniani ambao uliruhusu mawasiliano ya haraka kati ya Ulaya na sehemu nyinginezo za dunia.

Uvunaji Karafuu

Asilimia kubwa ya watu wa visiwa walishiriki katika mavuno ya karafuu ya msimu. Kawaida ya muda maalum wa mavuno na idadi kubwa ya wavunaji iliyohitajika ilisababisha sehemu ya mavuno haya, kwa nyakati fulani, kuwa uwanja wa migogoro ya vibarua.

Garifahari la Farasi la Sultan

Inasemekana kuwa garifahari hili la Farasi lilikuwa ni zawadi kutoka kwa Malkia Victoria.