Bustani za Victoria
Bustani hizi zilibuniwa na kupandwa na wataalamu wa kiGoa na zilitolewa kwa jiji na Seyyid Hamoud mwaka 1899. Zilizopo karibu na njia kuu kuelekea jijini bustani hizo zilitumika kama sehemu ya kukutania na kupumzika ya watu wa daraja la juu.
Barabara ya Mizigani
Barabara hii ya upande wa bandari imekuwa siku zote ni kiungo kikuu katika Mji Mkongwe.
Garimoshi la Bububu
Garimoshi hili lilifanya kazi kwa chini ya miaka 20 lakini lilikuwa linapendwa sana na lilitumiwa sana na abiria. Hata hivyo upungufu wa misafara ya kutosha ya mizigo ulilifanya liwe ghali sana. Mipango ya kuliendeleza kuelekea upande wa kaskazini wa kisiwa haikufika mbali kulingana na Upimaji Ardhi na Ramani ya Njia.
Njia za Mjini na Boti
Mwonekano wa mchoro kwa nyakati fulani hukolezwa katika baadhi ya kazi za mwanzoni za deLords.
Studio ya de Lord
Uendelezaji mdogo binafsi haukuathiri biashara ya picha, deLord alifungua duka katika sehemu iliyoonekana zaidi aliyoweza kuipata.
Duka la Tende
Ununuzi wa vitu maranyingi kwa pande zote mbili ni kazi na shughuli ya kijamii Zanzibar.
Wasichana wa kiSwahili
DeLord alitumia rangi kupata mvuto wa kutosha wa mitindo ya mwaka 1910.
Jengo la Makazi na Zahanati ya Kifaransa
Jengo kwa upande wa kushoto kabisa, hapa linatambuliwa kama Hospitali/Zahanati ya Kifaransa, baadaye likawa ni shule ya Mt. Joseph halafu likawa ni shule ya Tumekuja.
Mkondo wa Darajani
Ukarabati wa meli ndogo na uungaji ulikuwa ni biashara yenye faida katika Zanzibar ya zamani.